Showing posts with label EPL. Show all posts
Showing posts with label EPL. Show all posts

Wednesday, December 27, 2017

Mawingu Tz

Hatimaye Liverpool Yamnasa Beki Mholanzi Iliyemsotea Kutoka Southampton


Hatimaye Liverpool imefanikiwa kumnasa beki Mholanzi, Virgil van Dijk ambaye ilimsubukia kwa kipindi sasa.


Van Dijk atasaini na kujiunga na Liverpool pale pindi tu dirisha la usajili la Januari, 2018 litakapofunguliwa na Liverpool imekubali kutoa kitita cha pauni million 75 kwa Southampton.

Saturday, December 23, 2017

Mawingu Tz

Arsenal 3-3 Liverpool, Lilikuwa Bonge La Game Wabovu Watupu Walivyokutana, Picha Hizi Hapa...



Arsenal (4-3-3): Cech; Bellerin, Koscielny, Monreal (Mustafi 46), Maitland-Niles; Wilshere, Xhaka, Ozil; Iwobi (Welbeck 78), Lacazette, Sanchez (Walcott 89).
Subs not used: Ospina, Kolasinac, Elneny, Coquelin.
Bookings: Iwobi.
Goals: Sanchez 53, Xhaka 56, Ozil 58.


Liverpool (4-3-3): Mignolet; Gomez, Lovren, Klavan, Robertson; Can, Henderson (Milner 11), Coutinho (Oxlade-Chamberlain 84); Salah, Firmino, Mane (Wijnaldum 80).
Subs not used: Karius, Alexander-Arnold, Lallana, Solanke.
Goals: Coutinho 26, Salah 52, Firmino 71.
Referee: Martin Atkinson.  
Attendance: 59,409











Friday, December 22, 2017

Mawingu Tz

Man U, Man City, Chelsea, Liver Zikiwasajili Mastaa Hawa Januari Itapendeza Zaidi



ZIMEBAKI siku chache kabla ya dirisha dogo la usajili kufunguliwa nchini England.
Wakati zikiwa zimeshabaki siku hizo chache, tayari kuna baadhi ya makocha ambao wameshatangaza kuingia sokoni ili kujaza nafasi ambazo zimeonekana kuwa na upungufu katika raundi hii ya kwanza na huku wengine wakieleza kuwa itakuwa ni kama kupoteza muda.
Wanaosema ni kama kupoteza muda ni pamoja na Arsene Wenger wa Arsenal, lakini mwenzake Jose Mourinho akionekana kulisubiria kwa hamu dirisha hilo la majira ya joto.
Pamoja na Wenger kutoa madai hayo lakini alishawahi kuwasajili nyota kadhaa kama vile Andrey Arshavin, Nacho Monreal, Theo Walcott na Mohamed Elneny.
Licha ya wawili hao kuwa na mawazo tofauti, wachambuzi wa masuala ya soka wamejaribu kuangalia ni wachezaji wapi wanaweza kuzisaidia timu kubwa tano endapo watafanikiwa kunasa saini zao katika dirisha hilo dogo litakapofunguliwa na ifuatayo ni orodha hiyo:-
  1. Arsenal: Julian Draxler
Wakati mpaka sasa suala la nyota wake wawili Alexis Sanchez na Mesut Ozil kuhusu mikataba yao bado halijapatiwa ufumbuzi, kocha Arsene Wenger na klabu yake ya Arsenal wanakabiliwa na tatizo la kusaka mbadala wao.
Ili waweze kulimaliza, kiungo wa Paris Saint-Germain, Julian Draxler ambaye wamekuwa wakimwinda kwa misimu kadhaa, sasa ni wakati mwafaka kwao kuongeza kasi ili aweze kuokoa jahazi endapo nyota hao wawili wataendelea kuweka ngumu kusaini mikataba mpya.
Tofauti na ugumu uliokuwapo siku za nyuma, lakini sasa Arsenal wanaweza kupata mteremko kutokana na usajili ambao PSG waliufanya majira haya ya joto ambao ulishusha vifaa kama Neymar da Silva na Kylian Mbappe ambao tayari wameshamfunika nyota huyo na hivyo endapo Arsenal wataongeza juhudi inaweza kuwa rahisi kwao wakamnasa.
  1. Chelsea: Lucas Moura
Baada ya kufanya vizuri msimu wake wa kwanza alipotua Chelsea, kocha Antonio Conte, kwa sasa anaandamwa na shutuma kutokana na timu hiyo kutokuwa na matokeo ya kuridhisha.
Shutuma hizo zinatokana na kuwa baada ya kumfukuza straika wake, Diego Costa na kubaki na mastaa Willian na Michy Batshuayi, jambo hilo halijamsaidia kitu. Kutokana na ujio wa dirisha hilo dogo la usajili, ni nafasi pekee kwa kocha huyo kuweza kutua mzigo huo wa lawama wa nyota wa zamani wa klabu hiyo, Frank Lampard, anaamini Muitaliano huyo atasajili wachezaji wenye ubora.
Pamoja na kwamba Chelsea imeshatumia kitita cha pauni milioni 70 kumsajili Alvaro Morata, lakini suala la kusajili straika linapaswa kupewa kipaumbele.
Kutokana na hali hiyo, straika ambaye anaweza kumsaidia kocha huyo ni Lucas Moura, ambaye msimu huu amecheza dakika chache akiwa na timu ya Paris Saint-Germain.
  1. Liverpool: Leon Goretzka
Huku wakati ikiwa imebaki miezi michache kabla ya mkataba wake na timu ya Schalke kumalizika, klabu kubwa za Ligi Kuu England zikiwamo Liverpool na Arsenal, zimeshaanza kuonesha nia ya kutaka kumsajili.
Hata hivyo, mpaka sasa hakuna klabu ambayo imeshaonesha nia ya dhati kusaka huduma ya staa huyo kama ilivyokwa Liverpool.
Wakati nyota wake, Emre Can na Philippe Coutinho, wanahusishwa kutaka kuondoka jambo la kumsajili kiungo huyo Mjerumani Reds wanatakiwa kuelekeza jitihada zao kwa nyota huyo.
Pia kutokana na kwamba Schalke imeshapoteza wachezaji wengi wakiondoka wakiwa huru, hawataweza kukataa kitita cha pauni milioni 30 ili kumzuia mchezaji huyo ambaye ameshaonesha dhamira ya kweli ya msimu ujao kutotaka kuvaa tena uzi wa klabu hiyo ya Ligi ya Bundesliga.
  1. Manchester City: Inigo Martinez
Licha ya kuwa msimu huu Man City kuonekana kuwa vizuri, lakini bado inaonekana kuwa na upungufu kwenye safu yake ya kiungo wa kati na hivyo ili iweze kutwaa ubingwa, inalazimika kulimaliza tatizo hilo kwa haraka.
Hii ni kutokana na kwamba pamoja na kuwa na wastani wa mabao 3.2 kwa kila mechi na safu ya mabeki wa nyuma kuwa imara, lakini haiwezi kulinganishwa na Manchester United kwa kukaba kuanzia katikati.
Tatizo hilo lilianza kuonekana baada ya kuumia wachezaji wake, Benjamin Mendy na John Stones ambapo Eliaquim Mangala na Vincent Kompany, wanashindwa kuziba vyema nafasi zao na hivyo ili waweze kuondokana nalo, itabidi Januari wajitose sokoni ili kusaka beki wa kati mwingine na si mwingine bali ni Mhispania, Inigo Martinez.
  1. Manchester United: Willian
Manchester United mara zote huwa hawataki utani wakati linapofika suala la usajili.
Hii ni kutokana na kwamba mashetani hao wekundu wameshawahi kuwaliza mahasimu wao kwa usajili wa nyota kama vile Robin van Persie, Juan Mata na Nemanja Matic katika miaka ya hivi karibuni.
Kwa mara nyingine tena Manchester United inatajwa kumwinda winga wa Chelsea, Willian ambaye ameshatwaa ubingwa wa Ligi Kuu England mara mbili.
Mashetani hao wekundu wanaweza kunasa saini ya staa huyo kutokana na kwamba, kwa sasa hana maelewano mazuri na kocha wake, Antonio Conte na hivyo Man Utd wanatakiwa kuachana na mipango ya kuwafukuzia Ivan Perisic ama Gareth Bale ili kuweza kumwachia nafasi Mbrazili huyo atue Old Trafford.
Kutokana na ubora wake ikilinganishwa na chipukizi waliopo Marcus Rashford na Anthony Martial, anaweza kumsaidia Jose Mourinho kupigania ubingwa dhidi ya mahasimu wao katika Jiji la Manchesterna Man City.

Thursday, December 21, 2017

Mawingu Tz

Hii Hapa Ratiba Nusu Fainali Ya EFL(Carabao Cup 2017)

Baada ya timu nne zilizoingia Nusu Fainali ya EFL Caraboa Cup hatimaye Droo ilifanyika usiku wa Jana na droo hiyo Kuamua.
Katika Droo Hiyo imezikutanisha Chelsea vs Arsenal wakati Manchester City watacheza dhidi ya Bristol City.
Chelsea walijihakikishia kuingia Nusu Fainali baada ya kuwapa kichapo Bournemouth wakati Kwa jana hiyo Hiyo Man United akikubali kichapo cha bao 2 kwa 1 kutoka kwa Bristol City.
Mawingu Tz

Swansea Yamfungashia Vilago Kocha Wake.

Klabu ya Swansea City, imemfuta kazi meneja wake Paul Clement kutokana na mwenendo mbovu wa klabu hiyo msimu huu.
Clement mwenye miaka 45 alichukua jukumu la kuiongoza Swansea, mwezi Januari mwaka huu na kuisaidia kutoshuka daraja na kumaliza katika nafasi ya 15 msimu uliopita.
Katika msimu huu mpaka sasa Swansea wamecheza michezo 18, na wameshinda michezo mitatu ya ligi wakiwa wanaburuza mkia kwa alama 12.
Mwenyekiti wa Swansea Huw Jenkins, ametoa taaarifa kwa kusema klabu imelazimika kufanya hivyo ili kuweza kuisaidia timu kufanya vizuri.

Wednesday, December 20, 2017

Mawingu Tz

Mourinho Aionyesha Jeuri Real Madrid Vita Ya Hazard

Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho ameamua kumfungia kazi mshambuliaji wa Chelsea, Eden Hazard kwa kutaka kumrudisha kwenye himaya yake.
Mourinho ameingia kwenye vita hiyo ya kutaka kumsajili nyota huyo, huku akijua kwamba tayari Chelsea imempandia dau baada ya kumuahidi kumpa mshahara wa Pauni 300,000 kwa wiki kwa mkataba wa miaka minne.
Ofa hiyo mpya ya Hazard itategemea na uamuzi wake kuendelea kubaki Stamford Bridge.
Hata hivyo, Mourinho amejikuta akipambana na timu vigogo za Real Madrid, PSG ambazo zimeshatua kumuwinda nyota huyo.

Tuesday, December 19, 2017

Mawingu Tz

Jinsi “Soda” Ilivyomkomaza Gabriel Jesus Na Sababu Ya Ushangiliaji Wake Wa Simu

Chupa ya Champagne ni ghali sana kwa kijana ambaye amezaliwa mtaani na hana uhakika kuhusu maisha, kwa kijana ambaye amesota sana katika mitaa ya Sao Paulo kama Gabriel Jesus hakika Champagne ndio ingekuwa bata yake.
Lakink Jesus amesema hapana Champagne sio kitu kama soda walizokuwa wakigombea mjini Sao Paulo na kusema kwamba soda hizo japo ni bei rahisi sana nchini kwao lakini ni tamy mara 10 kuliko mivinyo hiyo.
Unajua nini kimezifanya kuwa tamu soda hizo? Ni jinsi zilivyopatikana kwani Jesus anasema ilibidi utumie jasho jingi,machozi hata na damu wakati mwingine ilu kupata chupa hiyo ya soda na ilikuwa fahari kwao.
Jesus anasema kulikuwa na mashindano ya mtaani ambayo yalichezwa katika viwanja vibovu na wakati mwingne barabarani na timu zilikuwa ngumu sana lakini mshindi wa mashindano hayo anapata soda.
Hilo lilimkomaza sana Jesus kisoka kwani alijituma sana yeye pamoha na wenzake kupata soda hizo na anakiri kwamba pale walipokuwa wakishinda walizunguka na soda hizo mtaa mzima wakiwaonesha watu ushindi wao.
Gabriel Jesus anasema akiwa na miaka 13 tu alianza kucheza na watu wakubwa ambao walikuwa wakimchezea rafu za makusudi na muda mwingine kumpiga kutokana na chenga zake na soka la maudhi.
Jesus hatasahau siku ambayo alikoswa na rafu mbaya na mtu aliyekuwa mkubwa kwake na baada ya mtu yule kunkosa Jesus aliamua kwenda nje ya uwanja ili amsubiri Jesus ampuge kutokana na kumpiga Chenga lakini Jesus anashukuru rafiki zake walimuokoa.
Gabriel anaamini mji wa Sao Paulo ulichangia sana yeye kukomaa kisoka na alipokwenda Amn City aliogopa sana na kuhisi anaweza kupoteza kila kitu kwani hakuwa anajua sehemu nyingine zaidi ya Sao Paulo.
Jesus anasema maisha ya Manchester yalikuwa ya upweke sana kwani alikuwa hamuoni mama yake wala marafiki zake na hii ikamfanya awe mpweke sana hali ambayo baadae alianza kuizoea.
Kuhusu ushangiliaji wake Jesus anasema huwa ana kaka yake ambaye kila akifunga goli humpigia simu pale mpira unapoingia tu nyavuni na ndio maana huweka vidole sikioni ishara ya kupokea simu ya kaka yake.
Tangu ajiunge City Jesus amefunga mabao 17 katika michezo 35, akifunga mabao 21 katika michezo 48 aliyoichezea Palmeiras huku akiifungia timu ya taifa ya Brazil mabao 8 katika michezo 13 aliyowachezea.
-Shaffih Dauda
Mawingu Tz

Man Utd Yamponza Lukaku….Akumbana Na Rungu La Polisi Nchini Uingereza

Mshambuliaji wa Manchester United, Romelu Lukaku ameamuriwa kulipa faini ya Pauni 384 baada ya kutuhumiwa kupiga kelele wakati akisherehekea kusajili Old Tafford msimu huu.
Hata hivyo, mshambuliaji huyo alipanga kufanya sherehe kubwa wakati wa kiangazi kusherehekea uhamisho wake lakini alilzamikia kuahirisha tafrija hiyo.
Raia huyo wa Belgium alitiwa hatiani na polisi wa usalama wa Marekani mwezi Julai kutokana na kudaiwa kupiga kelele kwenye nyumba ambayo alikuwa amepanga Baverly Hills.
Wakili Robert Humphries anayemtetea nyota hyo alisema, “Lukaku amekiri na kuomba radhi kwa yale yote yaliyotokea Beverly Hills.”
Mawingu Tz

ANATISHA:Mohammed Salah Avunja Rekodi Hii Ya Hatari


Bao la Mohammed Salaha dhidi ya Bournemouth limemfanya kuwa mchezaji wa kwanza wa Liverpool kufunga mabao 20 kabla ya Krismass tangu 1986.
Rekodi hiyo iliwekwa na gwiji wa zamani wa Liverpool, Ian Rush ambaye ameichezea klabu hiyo mechi 400.
Salah yuko katika nafasi nzuri ya kuelekea kuisaka rekodi ya Rush ya mabao 346 katika mashindano yote, mfungaji wa bora wa muda wote wa Liverpool.
Mshambuliaji huyo wa Misri kwa sasa anaongoza katika orodha ya wafungaji wa Ligi Kuu England akiwa na mabao 13, katika mechi 18 alizocheza.
Katika dakika1238, amekuwa na wastani wa kufunga goli kila baada ya dakika 99, hiyo ni maana amekuwa akifunga bao kila mechi.
Mo Salah amefunga mabao sita katika mashindano ya Ulaya hadi sasa msimu huu akiongoza Liverpool kufuzu kwa hatua ya mtoano wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Mchezaji wa mwisho kufunga mabao 20 kwa msimu katika kikosi cha Liverpool ni Luis Suarez.
Baada ya Salah kushindwa kutamba Chelsea watu waliohoji kuhusu uwezo wake.
Chelsea ‘Blues’ ilimtoa kwa mkopo Fiorentina na baadaye Roma, ambako alibadilika na kuonyesha uwezo wake wa kufunga na kumiliki mpira.

Monday, December 18, 2017

Mawingu Tz

Matokeo,Msimamo Na Orodha Ya Wafungaji Bora Ligi Kuu England(Uingereza).



Sunday, December 17, 2017

Mawingu Tz

Manchester United Yashinda, Lukaku Atupia Apotezea Kushangilia

Wachezaji wa Manchester United. 
Manchester United haijakata tamaa katika kuifukuzia Manchester City kwenye mbio za ubingwa wa Premier League baada ya kupata ushindi wa mabao 2-1.
Ushindi huo unaifanya Man United kupunguza pointi kati yao na Man City kwa kuwa pointi 11 badala ya 14 kama ilivyokuwa awali baada ya Man City kuifunga Tottenham Hotspur, juzi.

Mabao ya Manchester United yaliwekwa wavuni na Romelu Lukaku dakika ya 35 na Jesse Lingard dakika ya 53, wakati lile la West Bromwich Albion liliwekwa wavuni na Gareth Barry katika dakika ya 77.
Mara baada ya kufunga Lukaku hakushangilia kama ilivyokuwa katika mchezo uliopita dhidi ya AFC Bournemouth ambapo alifunga na hakushangilia.
Mawingu Tz

Matokeo Na Msimamo Wa Ligi Kuu England 2017/2018


Mawingu Tz

Klopp Aeleza Alivyotaka Kuacha Kumsajili Salah Hadi Alipolazimishwa

Kocha Jurgen Klopp wa Liverpool amefunguka kwamba aliingia hofu kumsajili Mohamed Salah hadi alipigwa presha.

Klopp amesema kitengo cha kusaka wachezaji cha Liverpool kilimpa presha kutaka Salah asajiliwe jambo ambalo alikuwa hakubaliani halo kwa hofu ya jumbo dogo la Salah.

Kocha huyo Mjerumani amesema, aliamini kwa jumbo la Salah kulikuwa na hofu ya kufanya vizuri Ligi Kuu England.

Wakati huo, wachezaji wake watatu ambao ni Philippe Coutinho, Sadio Mane na Roberto Firmino, aliamini wangebadilika na kumbeba.

Baadaye alikubali na Liverpool iliilipa AS Roma kitita cha pauni million 34 hali ambayo pia ilizua mjadala.

Lakini tayari Salah ametupia mabao 19 katika michuano tote akiwa na Liverpool na sasa winga huyo anaonekana ni tegemeo.

Salah ambaye ni mchezaji bora wa Afrika kupitia BBC ndiye anayeongoza kwa upachikaji wa mabao katika Ligi Kuu England akiwa na mabao13.
Mawingu Tz

Man City Haikamatiki, Yaipiga Tottenham Hotspur Mabao 4-1

Kevin De Bruyne katikati akishangilia na wenzake.
NI kama haina mpinzani katika Ligi Kuu ya England kwani Manchester City jana usiku iliifunga Tottenham Hotspur mabao 4-1 na kujiimarisha kileleni mwa Premier League.

Ushindi huo umeifanya Man City inayonolewa na Pep Guardiola kufikisha pointi 52 huku anayefuatia Manchester United akiwa na pointi 38. Man United leo inacheza na West Brom katika ligi hiyo. Spurs imebaki na pointi 31 na imeshuka hadi naafsi ya saba.
Mabao ya Man City yalifungwa na Ilkay Guendogan dakika ya 14 baada ya kupokea pasi ya Leroy Sane huku bao la pili likifungwa na Kevin De Bruyne akimalizia pasi ya Guendogan. Bao la tatu lilifungwa na Raheem Sterling dakika ya 80, Sterling alifunga bao la nne dakika ya 90. Spurs ilipata bao lake dakika ya 90 mfungaji akiwa ni Christian Erikssen


Gabriel Jesus akijiandaa kuingia Uwanjani.
Man City imeendeleza rekodi ya kutofungwa msimu huu kwani hadi sasa imecheza mechi 18 ambapo imeshinda mara 17 na kutoka sare mara moja.
MSIMAMO TOP FIVE PREMIER
P W D L Pts
1.Man City 18 17 1 0 52
2.Man United 17 12 2 3 38
3.Chelsea 18 12 2 4 38
4.Arsenal 18 10 3 5 33
5.Burnley 18 9 5 4 32

Friday, December 15, 2017

Mawingu Tz

Man City Yavunja Rekodi Ya Arsenal

Wachezaji wa timu ya Manchester City.
USHINDI wa mabao 4-0, dhidi ya Swansea City umeifanya Manchester City kuvunja rekodi ya Arsenal ya kushinda mechi nyingi mfululizo katika Premier League.

Man City sasa imeshinda mechi 15 mfululizo na kuivuka Arsenal ambayo ilikuwa ikishikilia rekodi ya kushinda mechi 14 mfululizo lakini yenyewe ilifanya hivyo katika misimu miwili tofauti wakati City wao wamefanikisha ndani ya msimu mmoja.

Pamoja na rekodi hiyo bado City ina nafasi ya kuweka rekodi zaidi ya hapo kwa kuwa inaendelea kucheza.
Kwa takwimu hizo pia Man City imekuwa timu ya nne kwa Ulaya kushinda mechi nyingi mfululizo katika ligi kuu.

Tuesday, December 12, 2017

Mawingu Tz

Maneno Ya Shombo Ya Wachezaji Man City Kwa Zlatan, Ndiyo Chanzo Cha Ngumi Kavu Man United Vs Man City






Maneno ya shombo ya wachezaji wa Manchester City, ndiyo yaliyosababisha mzozo na wenyewe kutwangana ngumi.

Hali ya wachezaji hao kutoelewana imeelezwa ilisababishwa na kauli iliyotoka katika kundi la wachezaji wa Man City waliokuwa wakipita mbele ya wachezaji wa Man United baada ya kushinda 2-1.

Mmoja wa wachezaji alimueleza Zlatan Ibrahimovic kwamba: “Zlatan, unachonga sana lakini hauna unalofanya.”

Ilikuwa tayari mchezo umeisha na baada ya hapo, ugomvi mkubwa uliibuka na kusababisha Kocha Msaidizi wa Man City, Mikel Arteta kupasuliwa katika paji la uso.


Man City ilifafanikiwa kutoka nyuma na kusawazisha mwisho kupata ushindi wa mabao 2-1.