Taarifa ambazo siyo rasmi kutoka ndani ya Klabu ya Simba zinaeleza kuwa klabu hiyo inampango wa kuachana na beki wake wa kati, Method Mwanjali.
Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zinaeleza kuwa maamuzi hayo yamefikiwa kutokana na mchezaji huyo mkongwe kuonekana kushuka kiwango huku kasi yake ikipungua siku baada ya siku.
Alipoulizwa Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara kuhusu suala hilo, alisema suala la usajili wao watalizungumza Jumatano hii ya Desemba 13 na kudai kuwa yanayozungumzwa kwa sasa ni tetesi tu lakini wao ndiyo watakaotoa tamko rasmi.
Tupe Maoni Yako