Tuesday, December 19, 2017

Mawingu Tz

ANATISHA:Mohammed Salah Avunja Rekodi Hii Ya Hatari


Bao la Mohammed Salaha dhidi ya Bournemouth limemfanya kuwa mchezaji wa kwanza wa Liverpool kufunga mabao 20 kabla ya Krismass tangu 1986.
Rekodi hiyo iliwekwa na gwiji wa zamani wa Liverpool, Ian Rush ambaye ameichezea klabu hiyo mechi 400.
Salah yuko katika nafasi nzuri ya kuelekea kuisaka rekodi ya Rush ya mabao 346 katika mashindano yote, mfungaji wa bora wa muda wote wa Liverpool.
Mshambuliaji huyo wa Misri kwa sasa anaongoza katika orodha ya wafungaji wa Ligi Kuu England akiwa na mabao 13, katika mechi 18 alizocheza.
Katika dakika1238, amekuwa na wastani wa kufunga goli kila baada ya dakika 99, hiyo ni maana amekuwa akifunga bao kila mechi.
Mo Salah amefunga mabao sita katika mashindano ya Ulaya hadi sasa msimu huu akiongoza Liverpool kufuzu kwa hatua ya mtoano wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Mchezaji wa mwisho kufunga mabao 20 kwa msimu katika kikosi cha Liverpool ni Luis Suarez.
Baada ya Salah kushindwa kutamba Chelsea watu waliohoji kuhusu uwezo wake.
Chelsea ‘Blues’ ilimtoa kwa mkopo Fiorentina na baadaye Roma, ambako alibadilika na kuonyesha uwezo wake wa kufunga na kumiliki mpira.

Tupe Maoni Yako