Mara baada ya Timu ya Taifa ya Tanzania Bara Kilimanjaro Stars kumaliza mchezo wa Raundi ya pili hatua ya Makundi CECAFA 2017 kwa kuchapwa na Ndugu zao Zanzibar Heroes bao 2 kwa 1 Licha ya Kilimanjaro Stars Kutangulia kupata Bao, Afisa Habari wa Timu ya Simba HAJI MANARA ameandika yafuatayo kupitia ukurasa wake wa Instagram.
” Sina shaka hata chembe.Zbar wakipata uanachama wa kudumu CAF na FIFA.watakwenda World Cup na Afcon kabla ya Tanzania Bara….najua wengine mtaudhika.ila hyo ni fact..wao 2 cc 1 ..hongera @zanzibarfootballassociation ”
Zanzibar katika mchezo huo walimaliza kipindi cha kwanza wakiwa nyuma kwa bao moja kwa sifuri kabla ya kurejea kipindi cha pili msomaji wa Kwataunit.com na kusawazisha bao kisha kuongeza bao la pili lililoipa Ushindi wa Pili baada ya Mechi ya Kwanza kushinda bao 3 kwa 1 dhidi ya Rwanda.
Tupe Maoni Yako