Maneno ya shombo ya wachezaji wa Manchester City, ndiyo yaliyosababisha mzozo na wenyewe kutwangana ngumi.
Hali ya wachezaji hao kutoelewana imeelezwa ilisababishwa na kauli iliyotoka katika kundi la wachezaji wa Man City waliokuwa wakipita mbele ya wachezaji wa Man United baada ya kushinda 2-1.
Mmoja wa wachezaji alimueleza Zlatan Ibrahimovic kwamba: “Zlatan, unachonga sana lakini hauna unalofanya.”
Ilikuwa tayari mchezo umeisha na baada ya hapo, ugomvi mkubwa uliibuka na kusababisha Kocha Msaidizi wa Man City, Mikel Arteta kupasuliwa katika paji la uso.
Man City ilifafanikiwa kutoka nyuma na kusawazisha mwisho kupata ushindi wa mabao 2-1.
Tupe Maoni Yako