Tayari makundi na ratiba nzima ya michuano ya soka ya kombe la dunia nchini Urusi imeshatoka, timi ya taifa ya Uingereza wapo katika Group G la michuano hiyo ambapo wapo pia na timu ya taifa ya Ubelgiji.
Waingereza wanafahamika kwa ukorofi wao pale ambapo timu yao ya taifa inacheza, na mara kadhaa mashabiki wa Uingereza wameingia katika matatizo na mamlaka za usalama katika mataifa mbalimbali waliyokwenda.
Mamlaka zinazohusika na masuala ya usalama nchini Urusi tayari zimejipanga kuwapokea Waingereza na tayari wameshawaonya kuhusu matukio ya kuhatarisha amani wakati wa michuano hiyo.
Mashabiki wa Uingereza wamekuwa na mtindo wa kuwashambulia mashabiki wa Urusi na kuimba nyimbo za kuwakashifu wao pamoja na viongozi wao jambo ambalo taifa la Urusi limesema halitakuwa tayari kuliona likitokea nchini mwao .
Kwa watakaofanya matukio kama hayo watakabiliwa na kifungo cha hadi miaka 15 nchini humo huku matapeli ambao wanauza tiketi feki wakikamatwa watapigwa faini kuanzi £3000 hadi £20000. Pia unywaji pombe hadharani katika michuano hiyo nao umepigwa marufuku.
Tupe Maoni Yako