Tuesday, December 19, 2017

Mawingu Tz

Man Utd Yamponza Lukaku….Akumbana Na Rungu La Polisi Nchini Uingereza

Mshambuliaji wa Manchester United, Romelu Lukaku ameamuriwa kulipa faini ya Pauni 384 baada ya kutuhumiwa kupiga kelele wakati akisherehekea kusajili Old Tafford msimu huu.
Hata hivyo, mshambuliaji huyo alipanga kufanya sherehe kubwa wakati wa kiangazi kusherehekea uhamisho wake lakini alilzamikia kuahirisha tafrija hiyo.
Raia huyo wa Belgium alitiwa hatiani na polisi wa usalama wa Marekani mwezi Julai kutokana na kudaiwa kupiga kelele kwenye nyumba ambayo alikuwa amepanga Baverly Hills.
Wakili Robert Humphries anayemtetea nyota hyo alisema, “Lukaku amekiri na kuomba radhi kwa yale yote yaliyotokea Beverly Hills.”

Tupe Maoni Yako