Showing posts with label YANGA. Show all posts
Showing posts with label YANGA. Show all posts

Friday, January 12, 2018

Mawingu Tz

Ajibu Aomba Radhi Yanga

Mshambuliaji wa Yanga, Ibrahim Ajibu.
BAADA ya kipigo cha penalti 5-4 dhidi ya URA, juzi mshambuliaji wa Yanga, Ibrahim Ajibu Migomba ameom­ba radhi kwa mashabiki wa timu hiyo kuto­kana na ma­tokeo ma­baya.

Yanga ilion­dolewa kwenye michuano ya Kombe la Map­induzi katika hatua ya nusu fainali na URA ya Uganda kutinga fainali dhidi ya Azam FC.

Msham­buliaji huyo alisema hawakupenda kupata matokeo ya aina ile lakini ilitokea vile kwa sababu mpira una matokeo matatu.

“Naomba mashabiki wetu wa Yanga wa­tusamehe kwa matokeo mabaya hakuna timu ambayo inapenda kupoteza zaidi mtupe sapoti ,”al­isema Ajibu.

Hata hivyo katika mchezo huo wachezaji ambao wali­piga penalti ni Papy Tshishim­bi, Hassan Kessy, Gadiel Michael, Daud Raphael na Obrey Chirwa ambaye alikosa.

Tuesday, January 9, 2018

Mawingu Tz

Chirwa Ang’oa Kigogo Yanga


SUALA la fungu lililobaki la usajili wa straika wa Yanga, Obrey Chirwa, limechukua sura mpya baada ya kigogo mmoja wa klabu hiyo kuamua kuachia ngazi, huku baadhi wakidai kuwa kigogo huyo ameamua kufanya hivyo kuepuka lawama.
Chirwa ambaye aliripotiwa kuomba ruhusa ya kwenda kwao Zambia kwa ajili ya matatizo yake ya kifamilia, lakini baadaye ilidaiwa amegoma kurejea Jangwani, akiwashinikiza mabosi wa Yanga kummalizia fedha zake za usajili.
Imedaiwa kuwa sababu ya straika huyo ‘kususa’ kurejea nchini ni kutokana na mvutano kati ya mchezaji huyo na uongozi wa klabu ambao unadaiwa kushindwa kummalizia fungu lililobaki kutokana na baadhi ya wajanja wachache kugawana kinyemela.
Habari zinasema wakati nyota huyo anasajiliwa mwaka 2016, tayari alishatengewa Dola 100,000 (zaidi ya Sh milioni 200 za Tanzania), lakini sehemu ya fedha hizo zilichotwa na wapiga dili.
Ni kutokana na mkanganyiko huo, inaelezwa kwamba tayari kigogo mmoja wa Yanga ameandika barua ya kuuacha wadhifa wake, sababu ikitajwa kuwa ni baada ya baadhi ya watu kumshutumu kuhusika na sakata la Chirwa.
DIMBA lilimtafuta Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Charles Boniface ‘Mkwasa’, ili kuthibitisha suala hilo lakini akasema hana taarifa hizo, japo taarifa kutoka Yanga zinadai kuwa ni kweli yupo kigogo aliyeamua kuachia ngazi.
“Siwezi kuthibitisha juu ya suala hilo kwa kuwa sijapata barua yoyote kutoka kwa kiongozi yeyote kujiuzulu na mimi juzi nilikuwa ofisini mpaka usiku,” alisema Mkwasa.
Akizungumzia kuhusu tetesi hizo za baadhi ya wajanja kumega fedha za Chirwa, Mkwasa alisema hana uhakika ila anachojua yeye ni kwamba mchezaji huyo ana madai yake na wanafanya taratibu za kumlipa.
Alipoulizwa juu ya ujio wa mchezaji huyo, Mkwasa alisema tayari yupo nchini tangu juzi usiku na sasa wanafanya jitihada za kumaliza tatizo lake ili aweze kujiunga na wenzake kwa ajili ya maandalizi ya michuano mbalimbali.
Kwa mujibu wa habari za ndani, Yanga walikuwa wanahaha kuhakikisha kuwa mchezaji huyo anarejea nchini, baada ya kumwambia kuwa madai yake yote yataisha baada ya yeye kuwasili nchini.
Taarifa zaidi kutoka Yanga zinadai kuwa mzigo mkubwa kwa sasa umemwelemea Mkwasa kwani anafanya kila linalowezekana kuhakikisha wachezaji wanalipwa mishahara yao huku ikidaiwa kuwa wapo wajanja wachache walioifanya klabu hiyo kuyumba.
Mawingu Tz

Chirwa Atinga Zenji Kuipa Yanga Ubingwa

WAKATI mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa, akitarajiwa kutua Zanzibar kukiongezea nguvu kikosi chake, Kocha Mkuu wa timu hiyo, George Lwandamina, ameelezea jinsi anavyotumia simu yake kumpa maelekezo msaidizi wake upande wa mazoezi ya viungo, Noel Mwandila.
Akizungumza na BINGWA kutoka nchini kwao Zambia jana, Lwandamina aliyeahidi kurejea nchini wiki hii kuendelea na majukumu yake baada ya kumaliza matatizo ya kifamilia yaliyokuwa yakimkabili, alisema japo hajawahi kuona mechi yoyote ya timu yake ya michuano ya Kombe la Mapinduzi inayoendelea Zanzibar, lakini amekuwa karibu mno na wasaidizi wake kuhakikisha mambo yanakwenda sawa.
“Nashukuru nimemaliza salama matatizo yangu ya kifamilia, nategemea kurejea huko wiki ya pili ya Januari,” alisema Lwandamina na kuongeza:
“Japo nipo mbali na timu, lakini nimekuwa nikiwasiliana na wenzangu huko Zanzibar kwa simu na kutoa ushauri pale inapolazimu kuhakikisha mambo yanakwenda sawa.”
Juu ya Chirwa aliyeelezewa kurejea nchini mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya kumalizana na klabu yake hiyo juu ya madai yake ya fedha za usajili, anaungana na wenzake Zanzibar kuongeza nguvu kuelekea mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya Singida United utakaopigwa leo.
Habari kutoka ndani ya Yanga zinasema: “Japo mimi si msemaji wa klabu, lakini ninachofahamu Chirwa anaondoka kesho (leo) asubuhi kwenda Zanzibar kuiongezea timu nguvu kwenye mashindano ya Mapinduzi ili timu iweze kutwaa ubingwa.”
Katika michuano hiyo, tayari Yanga imejihakikishia kutinga hatua ya nusu fainali baada ya kujikusanyia pointi tisa kutokana na mechi tatu, ambapo mchezo wao wa leo dhidi ya Singida utakuwa ni wa kuwania uongozi wa Kundi B.

Monday, January 8, 2018

Mawingu Tz

Tambwe Arejeshwa Dar Kwa Matibabu

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Mrundi Amissi Joselyn Tambwe amepanda boti mchana huu visiwani Zanzibar kurejea Dar es Salaam kwa ajili ya matibabu.
Daktari wa Yanga SC, Edward Bavu amesema leo kwamba Tambwe amelazimika kuondoka kambini mjini Zanzibar kurejea Dar es Salaam kwa  ajili ya matibabu zaidi ya Malaria.
“Ana Malaria, kwa siku zaidi ya nne sasa amekuwa na wakati mgumu, tumelazimika kumrejesha Dar es Salaam ili apatiwe matibabu zaidi,” amesema Dk. Bavu
Tambwe anaondoka wakati Yanga SC leo inateremka Uwanja wa Amaan, Zanzibar kumenyana na Singida United kuanzia Saa 2:15 usiku.Mrundi huyo amekuwa katika msimu mgumu, akianza kukaa nje tangu Agosti kutokana na maumivu ya goti kabla ya kurejea Desemba, lakini mapema Januari hii tena anaondolewa kambini kwa sababu ya Malaria.

Na hii inazidi kuipunguzia nguvu safu ya ushambuliaji ya Yanga kipindi hiki ambacho inawakosa wakali wake wengine wazoefu, Mzimbabwe Donald Ngoma na Mzambia, Obrey Chirwa. 
Yanga sasa itaendelea kumtegemea Ibrahim Ajib pekee katika washambuliaji wazoefu kwenye hatua iliyobaki ya Kombe la Mapinduzi – zaidi ya hapo ni chipukizi akina Yohanna Oscar Nkomola, Juma Mahadhi na Matheo Anthony.  

Mawingu Tz

Kamusoko Aendelea Na Mazoezi Dar, Moja Ya Kazi Ni Kupunguza Uzito

Kiungo Thabani Kamusoko ameendelea na mazoezi ya kurudi fiti ikiwa ni pamoja na kupunguza uzito.

Kamusoko ambaye alianza mazoezi taratibu wakati Yanga ikijiandaa na kwenda katika michuano ya Mapinduzi, moja ya sharti alilopewa ni kupunguza uzito.

"Kamusoko yuko Dar es Salaam, anaendelea na mazoezi mbalimbali yakiwemo ya kupunguza uzito, tukirejea tunaweza kuungana naye," alisema mmoja wa viongozi.

Kiungo huyo amekuwa nje ya uwanja kwa takribani miezi miwili na ushee akiuguza maumivu ya goti lake.

Tuesday, January 2, 2018

Mawingu Tz

MPYA : Kikosi Cha Yanga Kitakachoshiriki Klabu Bingwa Afrika


Mawingu Tz

Msikie Yule Straika Aliyewaliza Yanga Kirumba


YULE straika wa Mbao FC, Habibu Kiyombo, aliyewafanyia Yanga kitu mbaya katika mechi yao ya Jumapili Uwanja wa CCM Kirumba amesema , anatamani awe mchezaji bora wa muda wote kama walivyo wakali Muargentina Lionel Messi na Mreno Christian Ronaldo.
Kiyombo ambaye ndiye aliyewafunga Yanga mabao yote mawili jana Jumapili walipocheza mchezo wa ligi kuu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
“Niliwahi kuwafunga bao moja kwenye mechi yetu ya mwisho ya ligi kuu, kwa hiyo hata jana Jumapili, nilitamani kuwafunga, jambo ambalo nimelitekeleza. Nawashukuru wachezaji na kocha wetu ( Mrundi Ettiene Ndayiragije) kwa kukamilisha malengo yetu,”amesema Kiyombo.
“Natamani kuwa mchezaji bora wa muda wote, mfungaji bora na timu yangu ili iwe nafasi nzuri kama wanavyofanya Messi na Ronaldo kule kwao, natamani sana hivyo nitazidi kupambana hadi nifanikiwe."
Mshambuliaji huyo ambaye tayari amefunga mabao 12, ambayo ni pamoja na ya FA na ligi kuu amesema, bado ushindani ni mkali kwa nyota wengine wanaopambana kusaka kiatu cha mfungaji bora hivyo hatakata tamaa hadi mwisho wa Ligi.
Mawingu Tz

Gadiel, Buswita Wakwama CAF


YANGA wamepeleka kikosi cha wachezaji 20 kwa Shirikisho la Soka Afrika (Caf), kitachoshiriki Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani huku saba majina yakikwama.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga, Dismas Ten, alisema hawajatuma majina ya wachezaji ambao hawakuwamo katika kikosi kilichopita.
Ten alisema mpaka jana mchana walikuwa wametuma majina ya wachezaji 20, lakini yakikosekana ya wale waliosajiliwa dirisha kubwa na dogo la msimu huu, wakiwamo makipa Ramadhan Kabwili na Youthe Rostand.
Wengine ni mabeki Gadiel Michael, Abdallah Shaibu na Feston Kayembe, kiungo mshambuliaji Pius Buswita na mshambuliaji Yohana Nkomola, lakini jina na Papy Tshishimbi likijumuishwa kwenye orodha iliyotumwa.
Tshishimbi ni miongoni mwa wachezaji wapya waliosajiliwa na Yanga katika dirisha kubwa la Ligi Kuu Tanzania Bara lililofungwa Agosti 6, mwaka huu.
Hata hivyo, alisema walishindwa kuwajumuisha wachezaji 27 katika orodha iliyopelekwa Caf kutokana na changamoto ya mtandao.
Ten alisema wanatarajia kuwaongeza wachezaji hao baada ya mtandao kutengamaa, ambapo mwisho wa kutuma usajili Caf ni kesho.
“Tulikuwa na changamoto ya mtandao ambayo imesababisha kutowajumuisha wachezaji saba, lakini jina la Juma Mahadh tumeliondoa katika orodha ya wachezaji tutakaowatumia katika mashindano ya kimataifa,” alisema.
Alisema mipango yao ni kufika mbali katika mashindano ya mwakani.
Katika hatua nyingine, alisema kuwa mshambuliaji wao, Obrey Chirwa, anatarajia kurejea leo akitokea kwao Zambia.
Ten alisema mshambuliaji huyo anatarajiwa kuungana na wenzake visiwani Zanzibar watakaoshiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi.

Friday, December 29, 2017

Mawingu Tz

Yanga Yapata Mdhamini Mpya, Story Kamili Hii Hapa

HUENDA zile shida ndogondogo zikapungua pale Jangwani kwa sasa baada ya mabingwa wa kihistoria wa Ligi Kuu Bara, Yanga kuwa katika hatua za mwisho za kusaini mkataba mnono na kampuni ya vifaa ya Macron kutoka Italia.
Yanga ambayo ina mataji 27 ya Ligi Kuu kibindoni tayari imefanya mazungumzo ya awali na kampuni hiyo na huenda ikasaini mkataba huo mapema wiki ijayo.
Macron tayari imesaini mkataba wa miaka miwili na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ambapo watakuwa wakitoa vifaa kwa timu zote za Taifa. Macron pia itawapa TFF Sh400 milioni kila mwaka kwa miaka yote miwili ya mkataba.
Licha ya kwamba Yanga inafanya siri, Mwanaspoti imepenyezewa taarifa kuwa nyota wa zamani wa timu hiyo, Aaron Nyanda ambaye yupo kwenye Kamati ya Masoko ya timu hiyo ndiye anayesimamia dili hilo. Nyanda ambaye ni Ofisa Masoko wa TFF, ndiye aliyekamilisha pia dili la Macron na shirikisho hilo.
Taarifa za uhakika ambazo Mwanaspoti imezipata ni kwamba Yanga itasaini mkataba wa miaka miwili na Macron ambapo pamoja na mambo mengine, itapewa dola 250,000 (Sh556 milioni) kila mwaka.

Mbali na hivyo, Yanga itakuwa ikipokea mgawo wa faida kutokana na mauzo ya jezi zake kutoka kwenye kampuni hiyo, hivyo kila mwezi inaweza kuvuta kiasi kinachofikia Sh90 milioni.
“Dili linaweza kukamilika ndani ya siku tano ama sita zijazo. Dili lote linasimamiwa na Aaron Nyanda ambaye ndiye amefanikisha hao jamaa kusaini pale TFF, si unajua yupo kwenye Kamati ya Masoko ya Yanga, hivyo anawasaidia,” alisema mtoa habari huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake.

Yanga kwa sasa ina udhamini wa SportPesa inayoipa Sh950 milioni kwa msimu huu, Azam TV wanaowapa Sh272 milioni pamoja na Maji ya Afya ambao wanawapa maji ya bure mazoezini na katika mechi.
Mkwanja huo huenda ukamaliza ukata uliopo klabuni hapo kwa sasa ikiwemo tatizo la kuchelewa kwa mishahara.
Pia, Yanga huenda sasa ikapata fedha za kuwalipa nyota wake wanaoidai klabu hiyo kama Beno Kakolanya aliyejitoa na Obrey Chirwa ambaye amegoma kurejea nchini, wote wakishinikiza kulipwa haki zao za kimkataba.
Mawingu Tz

Yanga Wakwea Pipa, Watua Mwanza Kusubiri Kazi Na Mbao Fc...

Kikosi cha Yanga kimewasili salama jijini Mwanza tayari kuwavaa Mbao FC katika mechi itakayopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, keshokutwa.

Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, wameondoka leo asubuhi na tayari wamewasili kwa safari hiyo ya saa moja na dakika 14 kutoka Dar es Salaam kwenda Mwanza.


Mbao FC tayari iko kambini ikijiandaa na mechi hiyo inayotarajiwa kuwa tamu na yenye mvuto.
Mawingu Tz

Mwinyi Aandika Barua Yanga Akitaka Aachwe, Afc Leopard Ya Kenya Ndiyo Chanzo


Beki wa kushoto wa Yanga, Mwinyi Haji ameiandikia barua klabu yake akitaka imuachie aende zake kutafuta maisha.


Haji ameindika barua akitaka Yanga imuachie aende kujiunga na klabu ya AFC Leopards ya Kenya ambayo tayari kumsajili.

Akizungumza na SALEHJEMBE, Haji amesema ameona hana nafasi ya kucheza katika kikosi cha Yanga, hivyo angependa kwenda kujiendeleza zaidi.

"Kama sina nafasi, maana yake sina msaada na sihitajiki. Hivyo kwa makubaliano mazuri bila ya kugombana acha niende nikajiendeleze.

"Kazi yangu ni soka na ninataka kujiendeleza. Siwezi kuendelea nikiwa benchi, hivyo Yanga nimewaandikia waniachie niwahi kujiunga na AFC Leopards," alisema.

Beki huyo alionyesha kiwango cha juu na kuisaidia Zanzibar Heroes kufika fainali ya Kombe la Chalenji lililomalizika wiki moja na ushee iliyopita.

Thursday, December 28, 2017

Mawingu Tz

Yanga Sc Waiwangia Simba Mchana Kweupee


HUENDA kauli hii ikawa na ukakasi mkubwa kwa mashabiki wa Simba lakini ndiyo hivyo tena, kwamba wameambiwa na wenzao wa Yanga kuwa kama wanataka ubingwa wowote inabidi basi wasubiri msimu ujao wa 2018/19, kwani msimu huu hawana chao.
Yanga wamefikia kutamka maneno hayo mazito baada ya kuwaona watani zao hao wa jadi wakitupwa nje ya michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC), wakikubali kichapo cha mabao 4-3 kutoka kwa Green Warriors kwa mikwaju ya penalti.
Simba ndio waliokuwa mabingwa watetezi wa michuano hiyo lakini wakajikuta wakipata aibu hiyo ya mwaka, kitendo kilichowafanya kuamua kumtimu kocha wao mkuu Joseph Omog na sasa wanahaha kutafuta mbadala wake.
Wakati Simba wao wakiangukia pua, watani zao hao wa jadi mwishoni mwa wiki iliyopita walijihakikishia kusonga mbele hatua inayofuata baada ya kuwashushia kipigo cha mabao 2-0, Reha FC ya Temeke mchezo uliochezwa Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.
Kitendo hicho kimewafanya Yanga kukenua wakijiapiza kwamba msimu huu watakomba makombe yote na kama Simba wana hamu ya kunyakua ubingwa wowote, wanatakiwa kusubiri mpaka msimu ujao wa 2018/19 kwani msimu huu una wenyewe.
Msimu wa 2016/17, Yanga walifanikiwa kunyakua makombe yote, yani lile la Azam maarufu kama FA na la Ligi Kuu na sasa wanasema msimu huu tena watafanya hivyo kitu ambacho kinawafanya Simba kuweweseka hasa baada ya kuutema ubingwa wao wa FA.
Kitu pekee kinachoweza kuwabeba Simba kushiriki michuano ya kimataifa msimu ujao ni kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu, lakini Yanga wamesema wanataka kutetea ubingwa wao, yaani wautwae mara ya nne mfululizo na kuvunja rekodi hiyo ikimaanisha Wekundu wa Msimbazi, wana mlima mrefu wa kupanda.
Baada ya mchezo dhidi ya Reha kumalizika, kocha msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa, alisema malengo yao ni kuhakikisha msimu huu wanawafurahisha tena mashabiki wao kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu na ule wa FA.
“Kwanza niwashukuru wachezaji wetu kwa jinsi walivyopambana mpaka kupata ushindi huu wa mabao 2-0, nadhani lengo letu ni kuhakikisha msimu huu tunafanya vizuri na kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu na hili Kombe la FA,” alisema Nsajigwa, kauli ambayo si nzuri kwa mashabiki wa Simba.
Mbali na kauli hiyo ya Nsajigwa, idadi kubwa ya mashabiki na wanachama wa kikosi hicho, wameshajihakikishia kwamba, Simba hawawezi kufanya lolote mbele ya timu yao.
“Simba kwishnei kabisa, yaani msimu huu watasubiri sana, wao kama wanataka ubingwa wasubiri msimu ujao wa 2018/19 kwani msimu huu Yanga tutaendelea kutesa, wameshatolewa kwenye kombe lao la FA, tena wakifungwa na timu ndogo sasa ndiyo Ligi Kuu wataweza,” walisikika wakisema mashabiki wa Yanga baada ya kushinda mchezo wao dhidi ya Reha FC.
Hata mitaani kwenye vijiwe mbalimbali mashabiki wa Yanga wanaamini Simba wamepoteza dira hasa kitendo cha kumtimua kocha wao mkuu, Joseph Omog, kinatajwa kwamba kutazidi kuwavuruga.
Yanga wanaamini watashinda michezo yao yote ya Ligi Kuu iliyobakia ikiwamo wa mwishoni mwa wiki hii dhidi ya Mbao FC, utakaochezwa Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza, huku wakiamini Simba wataanza kupoteza dira dhidi ya Ndanda FC na kushuka kileleni.

Wednesday, December 27, 2017

Mawingu Tz

Kocha Morocco wa "Zanzibar" azungumzia tetesi za Kutua Yanga,Vipi Stars?

Kocha Mkuu wa ” Zanzibar Heroes ” Hemed Morocco ambaye amejizolea umaarufu mkubwa kufuatia soka safi la timu yake ya Taifa ya Zanzibar akisimama kama kocha mkuu kwenye timu hiyo ya Taifa.
Kwasasa kulikuwa na tetesi mbili kubwa zikimhusisha Hemed Morocco moja ikiwa ya nje ya nchi na nyingine ikiwa ni ya Hapa Hapa Tanzania.
Ya Nje ya Nchi msomaji wa Kwataunit.com ni ile ya kufundisha soka katika timu ya taifa ya Sudani Kusini na ya Ndani ikitajwa kuwa ni ya Yanga.
Akiongelea kama kuna timu yoyote imeshamfata nchini (Tanzania) Hemed Morocco amesema Hakuna timu iliyomfata na kufanya naye mazungumzo Tanzania mpaka sasa.
Na Kuhusu Sudan Kusini.
Morocco amesema ni kweli Sudan Kusini viongozi wa timu hiyo ya taifa walimfata wakati wa michuano ya CECAFA na wakafanya naye mazungumzo kuhusu uwezekano wa yeye kwenda kufundisha soka Sudan Kusini.
Amesema kuwa baada ya kumfata walifanya mazungumzo naye ya awali lakini mpaka sasa hakujawa na mawasiliano serious lakini kama wakitaka kufanya naye kazi yeye yuko tayari kwenda kwani kwasasa anatamani kufanya kazi Nje ya Nchi.
Morocco msomaji wa Kwataunit pia amewahi kuifundisha Stand United akiliongelea suala la Kama yupo tayari kufundisha Taifa Stars amesema kwasasa hawezi kuongelea suala hilo.

Mawingu Tz

Buswita Aanza Mikwara Yanga

Kiungo wa ti,mu ya Yanga Pius Buswita.
BAADA ya kufunga bao lake la pili tangu atue Yanga, kiungo mshambuliaji wa timu hiyo amewaambia mashabiki wa timu hiyo: “Tulieni, mbona mtafurahi sana.” Kauli hiyo, aliitoa wikiendi iliyopita mara baada ya kuifungia timu yake bao la kuongoza akipokea pasi ya Mrundi, Amissi Tambwe wakati Yanga ilipovaana na Reha FC katika mechi ya Kombe la FA iliyochezwa Uwanja wa Uhuru jijini Dar.

Kiungo huyo, hilo ni bao lake la pili kulifunga tangu ametua kuichezea Yanga kwenye msimu huu wa Ligi Kuu Bara akitokea Mbao FC ya Mwanza. Akizungumza na Championi Jumatano, Buswita alisema anafahamu mashabiki wa Yanga wanapenda kumuona akionyesha kiwango cha juu zaidi ya hicho amekionyesha kwa kifupi, hivyo ameomba muda kidogo.

Buswita alisema, ana mfupi tangu ametua kuichezea Yanga, hivyo kikubwa mashabiki wamvumilie huku akiendelea kuwathibitishia ubora wake taratibu kwenye mechi zijazo za ligi kuu na mashindano mengine. “Kikubwa watu wanatakiwa wafahamu kuwa, mimi nimetoka kwenye timu ndogo ya Mbao na nimekuja kwenye timu kubwa ya Yanga yenye presha kubwa ya mashabiki.

“Hivyo, ni lazima nibadilike taratibu kutoka mfumo niliokuwa nautumia nikiwa na Mbao na kuuchukua huu wa Yanga, hivyo siyo kazi ndogo inayohitaji muda kidogo wa mimi kuushika, pia kuzoeana na wenzangu. “Niwaahidi Wanayanga kuwa, mtafurahi na kunielewa wenyewe, kwani ninaamini uwezo wangu wa ndani ya uwanja ikiwemo kufunga na kutengeneza nafasi za kufunga mabao,” alisema.
Mawingu Tz

Himid Mao huyooo Yanga

SASA ni rasmi kuwa kiungo wa Azam, Himid Mao ‘Ninja’, anaweza kutua Yanga iliyokuwa ikimsaka kwa muda mrefu baada ya mchezaji huyo kushindwana na timu aliyokwenda kujiunga nayo ya Bidvest West ya Afrika Kusini.
Yanga ilikuwa ikimwania Mao tangu msimu uliopita, ikimwona kama suluhisho katika nafasi ya kiungo mkabaji.
Baada ya kumkosa, ilipiga hodi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na kumtwaa Papy Tshishimbi aliyeonyesha kiwango cha hali ya juu na kuwa kipenzi cha mashabiki wa Wanajangwani hao.
Moja ya sababu iliyowafanya Yanga kumkosa Mao, ni mpango wa kiungo huyo kwenda kucheza soka la kulipwa Afrika Kusini.
Lakini habari zilizopatikana jijini Dar es Salaam jana, zinasema kuwa Mao ameshindwana dau na Bidvest West na hivyo amerejea nchini kuendelea na maisha yake ndani ya Azam.
Kwa hali hiyo, iwapo Yanga wataendelea kumuhitaji, wanaweza kumtwaa mwishoni mwa msimu.
Chanzo cha kuaminika cha BINGWA kutoka ndani ya Azam, kinasema: “Kuna asilimia 75 za Himid Mao kubaki Azam kwani alipokwenda ‘South’ (Afrika Kusini) kwenye mazungumzo na klabu ya Bidvest, walishindwana katika suala la ‘mtonyo’ (fedha), hivyo msimu huu atabaki Azam, msimu ukimalizika anaweza kwenda timu nyingine lakini si Bidvest West tena.”
BINGWA lilimtafuta Mao kuzungumzia hilo ambapo alisema: “Nikweli nilikuwa Afrika Kusini, lakini siwezi kutaja ni klabu gani, pia sikuwa nimekwenda kwa lengo la kufanya majaribio kwani majaribio nilishafanya muda mrefu, nilienda kwa ajili ya mazungumzo na yamekwenda vizuri.”
Mao ni miongoni mwa viungo hodari wakabaji hapa nchini akiwa pia ni nahodha na tegemeo la timu ya Taifa, Taifa Stars.
Mawingu Tz

Hakuna Kingine Anachotaka Tambwe Ndani Ya Yanga Zaidi Ya Hiki Hapa..

Straika Mrundi wa Yanga, Amissi Tambwe aliyekuwa majeruhi kwa kipindi kirefu ameibuka na kufunguka kuwa amerejea kwenye makali yake.

Tambwe ambaye alikuwa nje kutokana na kusumbuliwa na goti lililomfanya akose mechi 11 za timu hiyo za ligi kwa mara ya kwanza Jumapili iliyopita alionekana uwanjani kwenye mchezo wa timu hiyo wa Kombe la Shirikisho (FA) dhidi ya Reha ambapo alihusika kwa kufunga bao moja katika ushindi wa mabao 2-0.

Mfungaji huyo wa Ligi Kuu Bara, mara mbili amesema mara baada ya kuonekana tena uwanja kwa sasa mtihani wa kwanza kwake ni kuhakikisha Yanga inakuwa na matokeo mazuri katika kila mchezo wake pamoja na kufunga mabao mengi tofauti na ilivyokuwa kwenye baadhi ya mechi.

“Nashukuru kwamba nimerejea ndani ya timu baada ya kupita kwa muda mrefu nikiwa nje kutokana na majeraha, na pia jambo la kushukuru ni kuwa nimeingia na kuiwezesha timu kupata matokeo kwenye mechi yetu iliyopita tena nikifunga na bao.


“Jambo ambalo lipo mbele yangu kwa sasa ni kuona kwamba Yanga inafanya vizuri kwenye kila mechi ya michuano tena na mimi nikiwa nafunga mabao, naamini yote hayo yatawezekana kwa sababu ya ushirikiano ambao nimeupata kwa wenzake mara baada ya kurejea tena uwanjani,” alisema mshambuliaji huyo.

Tuesday, December 26, 2017

Mawingu Tz

Mtoto Wa Lwandamina Alikunywa Sumu Baada Ya Tukio Hili La Kusikitisha


Mtoto wa Lwandamina alikunywa Sumu baada ya Tukio hili la Kusikitisha
Wakati wanachama, washabiki na wapenzi wa Yanga wakimsubiri kocha wao George Lwandamina kurejea Yanga kuendelea na Majukumu yake walipokea taarifa kuwa kocha huyo amefiwa na mwanaye Copa Mofya Lwandamina aliyedaiwa kufa kwa Kunywa Sumu.
Kupitia mtandao wa Futaa Zambai umeeleza Chanzo cha Kifo cha Mtoto wa Lwandamina Copa.
Inadaiwa siku ya tukio Copa (Mtoto wa Lwandamina) akiwa na rafiki yake Keith Chemu walikuwa wamekunywa pombe na Kulewa ndipo walimvaa mpangaji wa nyumbani kwao Aliyejulikana kwa jina la Hellen.
Walimvamia na Kumbaka na Kisha kumwibia simu na kiasi cha Shilingi 90000 za Kitanzania na wakampiga wakijua wameshamuua.
Baada ya muda mtoto wa Lwandamina alipata taarifa kuwa binti huyo mwenye Miaka 25 alikuwa hajafa na alikuwa hospitali na taarifa zilikuwa zishafika polisi na punde angeanza kutafutwa.
Hali ya taarifa hiyo ilimfanya Copa Lwandamina miaka 28 kuogopa na kuamua kuchukua maamuzi ya Kunywa Sumu.

Rafiki yake Keith Chemu waliyefanya naye tukio  kwasasa anashikiliwa na jeshi la polisi huko Lusaka Zambia katika jela ya Godfrey Chitalu akiwa kama Mahabusu kwa kosa la Kubaka na kujaribu kuua.
Hata hivyo inaelezwa kuwa hali ya binti Hellen  aliyekuwa na hali mbaya akiwa na alama shingoni na maumivu ya maeneo mengine kutokana na kupigwa inaelezwa kuwa anaendelea vizuri.
Mawingu Tz

Yule Mkongo Mpya Wa Yanga, Ameanza Kuutibua Uongozi Wa Klabu

Uongozi wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara, Yanga unaonekana kukerwa na kutorejea mapema kwa beki wao, Fiston Kayembe raia wa DR Congo ambaye alienda kwao lakini hadi jana Jumapili asubuhi alikuwa hajarejea akiwa amepitiliza muda aliopewa.

Kayembe aliyesajiliwa na Yanga kwenye dirisha dogo la usajili lililofungwa hivi karibuni akitokea Balende FC ya DR Congo, kwa mkataba wa miaka miwili, aliruhusiwa na uongozi wa timu hiyo kurejea kwao Congo kwa ajili ya kwenda kutatua matatizo ya kifamilia lakini mpaka jana asubuhi hakuwa amerejea.

Chanzo kimesema,  Mcongo huyo anawaumiza vichwa viongozi hao kutokana na kitendo chake cha kuwa kimya kurejea kuichezea timu hiyo licha ya muda ambao alipewa kwenda kwao kuisha tangu wiki iliyopita.

“Unajua kwamba huyu Kayembe ambaye tulimsajili hivi karibuni amewafanya viongozi waumie vichwa kwani tangu aliporuhusiwa kwenda kwao mpaka leo bado hajarejea licha ya kwamba anajua muda wake umeshaisha na anatakiwa awe amerejea.

“Na kitu kibaya ni kwamba hajatuma taarifa yoyote ile kwa viongozi ya kuonyesha kwa nini amechelewa ingawa alipoondoka hapa alienda kwenye matatizo ya familia yake, mpaka sasa haijulikani ni kipi ambacho kinamuweka huko lakini atakaporejea kila kitu kitajulikana,” kilisema chanzo hicho.


Meneja wa timu hiyo, Hafidh Saleh ambapo alisema: “Hilo suala lipo kwenye uongozi, mimi sihusiki nalo ila mchezaji huyo hajafika mazoezini.”

Saturday, December 23, 2017

Mawingu Tz

USAJILI : Mido La Kutisha Lililoyetinga "first eleven" CECAFA Laitaja Yanga

USAJILI : Aliyetinga ” first eleven ” CECAFA aitaja Yanga
Kiungo wa timu ya Taifa ya Zanzibar ” Zanzibar Heroes ” Abdulaziz Makame amefunguka Juu ya kama Yanga wanamwitaji kumsajili na Kusema yeye yuko tayari.
Makame aliyeng’ara sana kwenye michuano ya CECAFA yaliyofanyika mapema mwezi Huu (December ) nchini Kenya katika miji ya Machakos na Kisumu kiasi cha kuvutia timu nyingi
Makame msomaji wa Kwataunit.com amesema yeye yuko tayari kucheza Yanga na kama kweli Yanga wanamtaka basi hata leo hii yeye yuko tayari kucheza timu hiyo.
Abdulaziz Makame alikuwa moja kati ya wachezaji waliochaguliwa kwenye kikosi bora cha mashindano ya CECAFA 2017 kutokana na kucheza mechi zote katika ubora wa hali ya Juu.
Hata hivyo katibu mkuu wa Yanga Boniface Mkwasa siku kadhaa zilizopita aliiambia kwataunit.com kuwa baada ya kumsajili Mkomola na Kayembe hawana mpango wa Kuongeza mchezaji mwingine ndani ya Kikosi chao.
Mawingu Tz

Yanga Imetangaza Kamati Ya Mchakato Wa Mabadiliko Kwenda Kampuni, Wamo Wataalamu Wa Uchumi, Wanasheria

Uongozi wa klabu ya Yanga kupitia kaimu Mwenyekiti wake, Clement Sanga, leo umetangaza kuteua rasmi Kamati ya mabadiliko.

Wafuatao ndiyo walioteuliwa

1. Alex Mgongolwa -  Mwenyekiti - Mwanasheria

2. Profesa Mgongo Fimbo - Mtaalam wa Katiba na Sheria za Ardhi

3. Meki Sadiki - Mkuu wa Mkoa Mstaafu

4. Mohamed Nyenge - Mchumi na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi na Fedha

5. George Fumbuka -  Mshauri wa Masuala ya Uwekezaji

6. Felix Mlaki - Mchumi na Mtaalam wa Masuala ya Fedha