Showing posts with label AZAM. Show all posts
Showing posts with label AZAM. Show all posts

Wednesday, December 27, 2017

Mawingu Tz

Himid Mao huyooo Yanga

SASA ni rasmi kuwa kiungo wa Azam, Himid Mao ‘Ninja’, anaweza kutua Yanga iliyokuwa ikimsaka kwa muda mrefu baada ya mchezaji huyo kushindwana na timu aliyokwenda kujiunga nayo ya Bidvest West ya Afrika Kusini.
Yanga ilikuwa ikimwania Mao tangu msimu uliopita, ikimwona kama suluhisho katika nafasi ya kiungo mkabaji.
Baada ya kumkosa, ilipiga hodi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na kumtwaa Papy Tshishimbi aliyeonyesha kiwango cha hali ya juu na kuwa kipenzi cha mashabiki wa Wanajangwani hao.
Moja ya sababu iliyowafanya Yanga kumkosa Mao, ni mpango wa kiungo huyo kwenda kucheza soka la kulipwa Afrika Kusini.
Lakini habari zilizopatikana jijini Dar es Salaam jana, zinasema kuwa Mao ameshindwana dau na Bidvest West na hivyo amerejea nchini kuendelea na maisha yake ndani ya Azam.
Kwa hali hiyo, iwapo Yanga wataendelea kumuhitaji, wanaweza kumtwaa mwishoni mwa msimu.
Chanzo cha kuaminika cha BINGWA kutoka ndani ya Azam, kinasema: “Kuna asilimia 75 za Himid Mao kubaki Azam kwani alipokwenda ‘South’ (Afrika Kusini) kwenye mazungumzo na klabu ya Bidvest, walishindwana katika suala la ‘mtonyo’ (fedha), hivyo msimu huu atabaki Azam, msimu ukimalizika anaweza kwenda timu nyingine lakini si Bidvest West tena.”
BINGWA lilimtafuta Mao kuzungumzia hilo ambapo alisema: “Nikweli nilikuwa Afrika Kusini, lakini siwezi kutaja ni klabu gani, pia sikuwa nimekwenda kwa lengo la kufanya majaribio kwani majaribio nilishafanya muda mrefu, nilienda kwa ajili ya mazungumzo na yamekwenda vizuri.”
Mao ni miongoni mwa viungo hodari wakabaji hapa nchini akiwa pia ni nahodha na tegemeo la timu ya Taifa, Taifa Stars.

Friday, December 22, 2017

Mawingu Tz

Yanga Yaikimbiza Simba Viwango Vya Ubora Afrika, Fifa

Unaweza ukabisha ila ndiyo ukweli. Klabu ya Yanga inaongoza kwenye viwango vya ubora vya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) dhidi ya watani zao Simba baada ya viwango vya ubora kuonyesha inashika nafasi ya 345 kwa ubora Afrika baada ya mechi zilizochezwa Desemba 17.
Wapinzani wao Simba wanashika nafasi ya 371 huku Azam nao wakiwa nafasi ya 365 kwenye viwango hivyo. Taarifa ya viwango hivyo inayopatikana kwenye mtandao wa footballdata base.com ilioshesha klabu ya Esperance de ndiyo inashika nafasi ya kwanza barani Afrika.

Wednesday, December 20, 2017

Mawingu Tz

Azam Fc Yapata Pigo….Kumpeleka Mbaraka Yusuf Afrika Kusini

Mshambuliaji Mbaraka Yusuf wa Azam FC atakwenda kupata matibabu nje ya nchi.

Msemaji wa Azam FC, Jaffar Iddi amesema uongozi wa klabu hiyo, baada ya kupata majibu ya vipimo vyake, kesho ataondoka nchini kwenda Afrika Kusini.

“Majibu yanaonyesha ameumia meniscus kama ambavyo nilieleza awali. Hivyo atakwenda Afrika Kusini kesho kwa ajili ya matibabu,” alisema.


Mbaraka aliumia wakati akiitumikia timu ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars wakati akiitumikia katika michuano ya Chalenji.

Awali kulikuwa na taarifa kwamba Azam FC ilimtelekeza, jambo ambalo baadaye lilikanushwa na klabu ya Azam FC kwamba imekuwa ikiendelea kufuatilia hali yake.

Tuesday, December 19, 2017

Mawingu Tz

Azam Fc Yaweka Sawa Kuhusiana Na Mbaraka Yusuf Kuumia Timu Ya Taifa





Klabu ya Azam FC imesema mshambuliaji wao, Mbaraka Yusuf amegundulika ana tatizo la mfupa laini wa goti.

Msemaji wa Azam FC, Jaffar Iddi Maganga amesema, Mbaraka amegundulika ana tatizo hilo la Meniscus baada ya kufanyiwa vipimo akiongozwa na daktari wa klabu hiyo, Juma Mwankemwa.

“Kwa hiyo matibabu yanaendelea na klabu ya Azam FC ndiyo inayoshughulikia, hivyo suala la kwamba ametelekezwa, hapana,” alisema.


Mbaraka aliumia wakati akiitumikia timu ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars katika michuano ya Chalenji iliyomalizika kwa wenyeji Kenya kubeba kombe dhidi ta Zanzibar Heroes kutoka Tanzania.

Wednesday, December 13, 2017

Mawingu Tz

Himid Mao Mbioni Kumalizana Na Timu Hii Ya Afrika Kusini

Wakati dirisha dogo la usajili likielekea kufungwa siku chache zijazo, kuna taarifa kadhaa kuhusu usajili wa wachezaji wa Tanzania.
Inadaiwa kuwa kiungo mkabaji wa Azam FC, Himid Mao, amefuzu majaribio ya kujiunga na Klabu ya Bidvest inayoshiriki Ligi kuu ya nchini Afrika Kusini na yuko mbio kwenda kumalizana naoHimid Mao – Tanzania.
Bado hakuna taarifa kamili kutoka Azam FC juu ya taarifa hizo za usajili.
Aidha, upande mwingine inaelezwa kuwa Muhsin Makame ambaye ni mshambuliaji wa Serengeti Boys amejiunga na Njombe Mji kwa mkopo akitokea Klabu ya Mtibwa Sugar ya mkoani Morogoro.

Tuesday, December 12, 2017

Mawingu Tz

Madrid Waanza Tamaa Kwa Salah, Yataka Kutoa Fedha Na Mchezaji Impate


Mavituuuz ya Mohamed Salah yanaonekana kuwachanganya matajiri Real Madrid ambao wameweka hadharani kwamba wanamtaka.

Tayari Salah aria wa Misri na mchezaji bora wa BBC, amefunga mabao 18 katika mechi za Ligi Kuu England na Ligi ya Mabingwa Ulaya.


Imeelezwa tayari thamani ya Salah aliyetokea AS Roma imefikia pauni million 39 na Madrid inaonekana inataka kumtwaa na pamoja na kuilipa Liverpool, itamtoa Lukas Vazquez.

Salah anaonekana kuwa ndiyo tegemeo la Liverpool katika ushambulizi kila siku zinavyosonga mbele.

Raia huyo wa Misri amekuwa tegemeo katika uchezaji wa timu, utoaji wa pasi za mabao na wakati mwingine kufunga mwenyewe.

Sunday, December 10, 2017

Mawingu Tz

Mshambuliaji Mpya Mghana, Arthur Aanza Balaa


KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, imetoka sare ya bao 1-1 na Friends Ranger katika mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenue Uwanja wa Azam Complex usiku wa jana.
Ilikuwa ni siku nzuri kwa mshambuliaji mpya wa timu hiyo Bernard Arthur, aliyekuwa akicheza mechi yake ya kwanza tokea asajiliwe akitokea Liberty Professional ya Ghana baada ya kufunga bao la kusawazisha dakika ya 68.
Mpira huoa ulikuwa ni mkali sana ambapo Azam FC ilicheza vema kipindi cha pili baada ya mabadiliko ya kuingia winga Enock Atta, kiungo Frank Domayo na mshambuliaji Wazir Junior.
Mshambuliaji mpya Mghana wa Azam, Bernard Arthur akikimbia kushangilia baada ya kufunga 

Friends Ranger ilijipatia bao lake dakika ya 65 kupitia kwa Mau Gola kufuatia uzembe uliofanyika kwenye safu ya ulinzi ya Azam FC kabla ya dakika tatu baadaye matajiri hao kusawazisha.
Azam FC iliutumia mchezo huo kama sehemu ya kuwapa ushindani wachezaji wake kutokana na kusimama kwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) kupisha michuano ya Kombe la Chalenji inayoendelea nchini Kenya.
Kikosi cha Azam FC jana kilikuwa; Mwadini Ally, Swaleh Abdallah, Hamimu Abdallah/Daniel Amoah dk 76, David Mwantika, Agrey Moris/Oscar Masai dk 86, Salmin Hoza, Braison Raphael/Enock Atta dk 66, Masoud Abdallah/Frank Domayo dk 61, Ramadhan Singano/Wazir Junior dk 61, Bernard Arthur/Paul Peter dk 70, Joseph Mahundi

Wednesday, December 6, 2017

Mawingu Tz

PICHAZ:Tazama Jinsi Mshambuliaji Mpya Wa Azam Alivyoanza Kuonesha Mavituz Huko Chamazi

Mshambuliaji mpya wa Azam FC, Bernard Arthur akiondoka na mpira katika mazoezi ya timu hiyo jana asubuhi Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam
Bernard Arthur amekuwa kivutio katika mazoezi ya Azam FC tangu awasili wiki iliyopita  
Bernard Arthur (kushoto) akikimbia na wenzake Azam Complex, Chamazi
Bernard Arthur hapa akifanya mazoezi ya gmy ndani ya Azam Complex
Wachezaji wengine wa Azam FC wanaendelea na mazoezi pia na hapa wakiwa kwenye bwawa la kuogelea la Azam Complex

Mawingu Tz

Msuva Anazidi Kuwa Matawi Ya Juu Aingia Kwenye Kikosi Bora Cha Mwezi Morocco

WINGA wa kimataifa wa Tanzania, Simon Happygod Msuva ameteuliwa kwenye kikosi bora cha mwezi cha Ligi Kuu ya Morocco baada ya kazi nzuri Novemba.
Msuva amefunga mabao mawili na kuseti matatu, Difaa Hassan El Jadida ikishinda mechi tatu na kupanda hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi ya Morocco, maarufu kama Botola.
Na baada ya mafanikio hayo, si ajabu Msuva anateuliwa kikosi bora cha mwezi Novemba chga Botola.
Msuva ameunza vizuri pia mwezi Desemba baada ya kuifungia bao moja Difaa Hassan El - Jadida ikishinda 4-1 dhidi ya Khouribga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Morocco Uwanja wa Ben Ahmed El Abdi mjini El Jadida, Mazghan Jumapili.
Msuva, mshambuliaji wa zamani wa mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga SC alifunga bao lake dakika ya 71, likiwa la nne katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya Morocco maarufu kama Botola.



Simon Msuva mstari wa pili kutika juu kulia katika kikosi bora cha Botola Novemba 
Mabao mengine matatu ya DHJ siku hiyo yote yalifungwa na mshambuliaji chipukizi Mmorocco, Hamid El Ahadad dakika za 30, 40 na 57.

Tuesday, November 28, 2017

Mawingu Tz

Ratiba Mapinduzi Cup Yatoka Hii Mpya Itazame..Simba,Yanga Patachimbika


SIMBA SC itafungua dimba na URA ya Uganda katika michuano maarufu ya Kombe la Mapinduzi, Januari 2, mwaka 2018 Uwanja wa Amaan, Zanzibar mchezo ambao utaanza Saa 2:15 usiku.
Mahasimu wao, Yanga wataanza na JKU ya Zanzibar Desemba 1, Uwanja wa Amaan pia, mchezo ambao nao utaanza Saa 2:15 usiku.
Mabingwa watetezi, Azam FC wataanza na Jamhuri katika mchezo utakaofanyika Uwanja wa Amaan pia Desemba 2, lakini kuanzia Saa 10:15 jioni. Ufunguzi rasmi wa Kombe la Mapinduzi 2018 utafanyika Desemba 30, mwaka huu kwa mechi mbili kuchezwa Uwanja wa Amaan, kwanza Zimamoto na Mlandege Saa 10:17 jioni na baadaye JKU na Shaba Saa 2:15 usiku.        

Simba imepangwa Kundi A pamoja na Azam FC, Jamhuri, Taifa ya Jang’ombe na URA ya Uganda, wakati Yanga imetupwa Kundi B pamoja na JKU, Mlandege, Zimamoto na Shaba.
Simba itamenyana na Azam FC Januari 6, ikitoka kukipiga na Taifa ya Jang’ombe Januari 4, kabla ya kumalizia mechi zake za Kundi A Januari 8 na Jamhuri.
Azam FC itacheza na Taifa ya Jang’ombe Januari 4 kuanzia Saa 10:15, kabla ya kumenyana na Simba na itahitimisha mechi zake za Kundi A kwa kuumana na URA Januari 8 Saa 10;15 pia jioni Uwanja wa Amaan.
Baada ya mechi na JKU, Yanga watarudi tena uwanjani Januari 3 kwa mchezo na Shaba, Januari 5 na Zimamoto kabla ya kukamilisha mechi zake za Kundi B kwa kumenyana na Mlandege Janauri 7 Uwanja wa Amaan.
Nusu Fainali zinatarajiwa kuchezwa Januari 10 na Fainali itakuwa Januari 13, mwaka 2018 Uwanja wa Amaan kuanzia Saa 2:15 usiku.

Monday, November 27, 2017

Mawingu Tz

Straika Mpya Hatari Wa Azam Atua Rasmi Tayari Kuanza Kufumania Nyavu

Bernard Arthur (katikati) akiwa Uwanja wa Ndege wa JNIA, Dar es Salaam na Mtendaji Mkuu wa Azam, Abdul Mohamed (kushoto) baada ya kuwasili leo

MSHAMBULIAJI mpya wa Azam FC, Bernard Arthur, amewasili asubuhi ya leo Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam tayari kuanza maisha mapya Chamazi.

Arther aliyesaini miaka miwili na klabu hiyo akitokea kwenye timu ya Liberty Professional ya kwao, Ghana, amewasili leo akiongozana na Mtendaji Mkuu wa Azam, Abdul Mohamed ambaye alimfuata nchini humo kukamilisha usajili wake.
Akizumgumza mjini Dar es Salaam leo, Ofisa Habari wa Azam, Jafari Idd alisema kuwa, mchezaji huyo tayari ameungana na timu huku akisubiri uongozi wa klabu hiyo wakishughulikia vibali yake kwa ajili ya kuanza kazi rasmi.


“Mchezaji wetu mpya wa Ghana, amewasili alfajiri ya leo nchini akiwa na Mtendaji mkuu wa Azam, Abdul Mohamed, tayari ameungana na timu Chamazi huku akisubiri uongozi kushughulikia vibali vyake ili aweze kuanza kazi rasmi,” alisema Jafari.

Usajili wa Arthur ni sehemu ya mapendekezo ya benchi la ufundi la timu hiyo kwenye usajili huu wa dirisha dogo, anayekuja kuziba pengo la straika mwingine, Yahaya Mohammed, aliyeondoka kwa makubaliano maalumu ya pande mbili wiki chache zilizopita.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa timu ya WAFA (Ghana) na Asec Mimosa ya Ivory Coast, anaungana na washambuliaji wengine wa timu hiyo katika kukiongezea makali kikosi hicho, ambao ni Mbaraka Yusuph, Wazir Junior, Yahya Zayd, Shaaban Idd pamoja na wale waliopandishwa kutoka Azam B, Paul Peter na Andrea Simchimba.
Wakati huo huo Jafari alisema timu inajiandaa kwa ajili ya mechi yao ya kesho dhidi ya Mtibwa Sugar a Morogoro, mchezo wa raundi ya 11 ya Ligi Kuu Bara utakaopigwa kuanzia saa moja usiku kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

Katika hatua nyingine, nyota wawili wa Azam FC, Shaaban Idd na Joseph Kimwaga, waliokuwa majeruhi sasa huenda wakarejea dimbani Januari Mosi mwakani wakati timu hiyo ikishiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar.
Mbali na kufanya programu ya mazoezi ya gym, Idd tayari ameruhusiwa kuanza mazoezi madogo madogo ya kucheza na mpira na kukimbia mwanzoni mwa wiki hii huku Kimwaga akiendelea na mazoezi ya gym aliyoanza mwezi mmoja uliopita.
Daktari wa Azam FC, Mwanandi Mwankemwa, amesema kwamba wachezaji hao wapo kwenye kipindi cha mwisho cha tiba yao cha kuwarejesha katika hali yao ya kawaida huku akidokeza Idd ataendelea na programu hiyo na anatarajiwa kurejea dimbani kuanzia Januari Mosi.“Kimwaga kidogo kumetokea matatizo kidogo katika ukunjaji wa goti lake baada ya operesheni kwa hiyo sasa hivi bado anafanya mazoezi ya kukunja goti na pindi atakapokuwa ameweza kukunja goti vizuri naye ataruhusiwa kuanza kucheza mpira kidogo kidogo na kukimbia naye pia tutamtarajia itakapofika Januari Mosi atarudi tena kiwanjani kwenye ushindani,” alisema.


Idd anasumbuliwa na majeraha ya nyonga yake ya mguu wa kulia huku Kimwaga akisumbuliwa na goti la mguu wa kushoto kwa pamoja walifanyiwa upasuaji nchini Afrika Kusini na tokea waanze mazoezi ya gym wamekuwa chini ya uangalizi wa daktari wa Azam FC na wataalamu wa Kliniki ya London Health Centre, iliyopo eneo la Macho, Msasani jijini Dar es Salaam wanakofanya mazoezi ya gym.

Mawingu Tz

Msimamo Ligi Kuu Tanzania Bara VPL 2017/2018

 

Thursday, November 16, 2017

Mawingu Tz

Tetesi Za Usajili Yanga Leo Jumamosi Novemba 11 2017 Wanaoingia Na Wanaotemwa Hawa Hapa

Viongozi wa Yanga wamefika bei kwa mshambuliaji wa Prisons, Mohammed Rashid aliyezaliwa mwaka 1995 wakati Tanzania ikifanya uchaguzi mkuu wa vyama vingi vya siasa.

Mpango wao ni kusajili mshambuliaji mmoja wa ndani na mwingine wa nje, sasa ndani upepo umeng'ang'ania kwa Mohammed ambaye Kocha George Lwandamina ameambiwa amuangalie kwa mara ya mwisho kwenye mechi dhidi ya Simba, Novemba 18 ndani ya Sokoine, Mbeya.

Mmoja wa viongozi mwenye ushawishi mkubwa ndani ya kamati ya usajili ya Yanga ameidokeza Mwanaspoti kuwa wao wanamkubali mchezaji huyo chipukizi na wamemuambia Kocha ajiridhishe kwenye mechi na Simba, akiwapa dole tu wanamaliza mchezo kwa gharama yoyote ile tena siku hiyohiyo.

Lwandamina ambaye anarejea nchini keshokutwa Jumatatu akitokea kwao alipokwenda kuhani msiba, atakutana pia na makali ya mchezaji huyo atakapoivaa Yanga Novemba 25 katika Uwanja wa Uhuru katika mechi ya ligi. Lakini huenda asifike kote huko kama mchakato wake ukimalizwa baada ya mechi na Simba.

"Hatutaki kumsajilia kocha kama ambavyo timu zingine zinavyofanya akisema hafai tutaanza kuangalia wale wa kigeni kutokana na hapa ndani hatudhani kama kutakuwa na kitu cha ziada tena kuzidi huyu wa Prisons,"alidokeza Kigogo huyo huku akitaka jina lake lisitokee gazetini kwasababu binafsi.

Lakini Mohammed ambaye huvaa jezi namba 10 ndani ya Prisons alipoulizwa na Mwanaspoti alisema; "Sipo katika nafasi nzuri ya kuzungumza chochote kuhusu kujiunga na timu hizo kubwa kwa sasa kwani hakuna ambayo imenifuata."

"Kikubwa kwangu ni kuendelea kujituma na kufanya vizuri zaidi. Mnaweza kusema nitafunga zaidi kama nitakuwa nacheza sambamba na Ibrahim Ajibu, Emmanuel Okwi ama Shiza Kichuya lakini hilo linategemea, lengo langu ni kufunga angalau mabao 15 msimu huu," alieleza mchezaji huyo aliyefunga mabao sita kwenye mechi tisa.

"Siwezi kusema kama wakinifuata nitakwenda ama la, hilo kwa sasa lipo nje ya uwezo wangu, natazama zaidi kazi yangu,siwezi pia kusema kama timu yangu ya Prisons ikiniruhusu nitakubali kwenda, hapana, ni ngumu kuwa na jibu la moja kwa moja sasa," anafafanua mchezaji huyo ambaye si askari Jela.

Mzambia huyo alinukuliwa na Mwanaspoti akisema kwamba anataka uongozi wake kumtafutia washambuliaji wawili wenye makali zaidi ya Ibrahim Ajibu na Obrey Chirwa wanaoibeba Yanga kwasasa.

Lakini habari za ndani zinadai kwamba kuna uwezekano Yanga ikafikiria kutengua mkataba wa mmoja kati ya Amissi Tambwe au Donald Ngoma ili kuingiza mashine moja ya kigeni.
source : Mwanaspoti
Mawingu Tz

Haya Hapa Makundi Ya CECAFA Challenge CUP Na Tarehe Ya Kuanza Mashindano

Tanzania Bara itafungua mashindano ya Kombe la Chalenji Desemba 3 kwa kuivaa Libya kwenye Uwanja wa Kisumu, Kenya.


Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa leo Alhamis na Baraza la Vyama vya Soka vya Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) ,Tanzania Bara imepangwa Kundi A pamoja na ndugu zake Zanzibar, Rwanda, wenyeji Kenya na Libya wakati Kundi B lina timu za Burundi, Ethiopia, Uganda, Sudan Kusini na Zimbabwe.

Libya na Zimbabwe zimealikwa kushiriki mashindano hayo baada ya Sudan na Somalia kujiondoa kwa sababu mbalimbali
Mawingu Tz

Wanaoachwa Simba, Yanga Hawa Hapa

WAKATI dirisha dogo la usajili likitarajiwa kufunguliwa Novemba 15, mwaka huu, timu kongwe za Simba na Yanga zimetajwa kutaka kutema baadhi ya wachezaji wao ili kuingiza maingizo mapya.
Timu hizo zinafahamu kwamba mwakani zinakabiliwa na michuano migumu ya kimataifa, na sasa zinataka kusafisha wachezaji ambao wanaonekana ni mizigo na kuingiza wapya wenye uwezo mkubwa.
Yanga, ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, wataiwakilisha nchi Ligi ya Mabingwa Afrika, wakati Simba wakishiriki michuano ya Kombe la Shirikisho, baada ya kukaa kwa misimu kadhaa bila kufanya hivyo.
Baadhi ya wachezaji ambao wanatajwa kwamba huenda wakakutana na panga kwa upande wa Yanga yupo Donald Ngoma pamoja na Mrundi Amis Tambwe, ambao msimu huu wameshindwa kufanya kile ambacho kilitarajiwa.
Ngoma amecheza michezo michache na baada ya hapo akatimkia kwao Zimbabwe bila ruhusa ya uongozi wala benchi la ufundi, ambapo wenye Yanga yao wamekasirika wakitaka aondoke asije akajifanya ‘Mungu mtu.’
Kwa upande wa Tambwe, tangu msimu huu uanze hajagusa nyasi za uwanja kutokana na majeraha aliyoyapata msimu uliopita na taarifa kutoka Yanga zinadai kuwa, wanafikiria kumtema ili asije akawagharimu mbele ya safari, ikizingatiwa kuwa, timu inashiriki michuano ya kimataifa.
“Ngoma yeye kuna asilimia kubwa ya kumtema kutokana na ukweli kwamba, anajiona yeye ni mfalme anaweza kufanya lolote, ndiyo maana amekwenda kwao bila taarifa kwa uongozi, kwa Tambwe dalili zinaonyesha naye yatamkuta makubwa, kwani majeraha yanaweza yakamsababishia kushindwa kushiriki vizuri Ligi ya Mabingwa.
“Lililopo ni kwamba, tunataka kusajili washambuliaji wazuri watakaoziba mapengo yao, kwani Yanga ni timu kubwa ambayo mashabiki wake siku zote wanataka matokeo mazuri,” alisema kigogo mmoja kutoka Yanga.
Wachezaji wengine ambao taarifa zinasema ama watatemwa jumla au kutolewa kwa mkopo ni kipa Beno Kakolanya, Juma Mahadhi na Matheo Anthony, ingawa mchujo bado unaendelea kwa wengine.
Kwa upande wa Simba, taarifa zinadai kuwa, beki Mzambia, Method Mwanjali na straika Mrundi, Laudit Mavugo, wapo kwenye hali tete na kamati ya usajili ambayo ilitarajiwa kukaa wikiendi hii, inaweza kutoka na jibu moja.
Taarifa kutoka ndani ya Simba zinadai kuwa, wanataka kumtema Mwanjali kwa kigezo cha umri, ambao wenyewe wanadai ndio unaosababisha achelewe kupona pindi anapoumia, huku Mavugo naye akidaiwa kutokuwa na ile kasi yake ya upachikaji mabao aliyokuwa nayo katika klabu yake ya Vital’O ya Burundi akiwa Simba.
Taarifa hizo zinadai kuwa, huenda Mavugo akatimkia kwa mabingwa wa Ligi Kuu nchini Kenya, Gor Mahia, ambayo inanolewa na kocha wa zamani wa Wekundu hao wa Msimbazi, Dylan Kerr.
Mbali na wawili hao, pia wapo wanaotajwa kwamba watatolewa kwa mkopo kwenye timu nyingine, akiwamo winga Jamal Manyate, Jamal Mwambeleko na Juma Luizio, ambaye inadaiwa kuwa ameweka bayana kwamba, anataka kupewa barua ya kutemwa akatafute maisha kwingine.
Baada ya taarifa hizo kutufikia tulimtafuta Katibu Mkuu wa Simba, Arnold Kashembe, ambaye alikiri kwamba kamati ya usajili inakutana ili kupitia ripoti ya benchi la ufundi na ndio watakaotoka na jibu la moja kwa moja.
“Hao wachezaji uliowataja (Mwanjali na Mavugo) kwamba wanatemwa hilo sina uhakika nalo, isipokuwa subiri mpaka kamati ya usajili itakapokaa na kumaliza kazi yake. Wenyewe wanaweza kukaa siku hizi mbili, naamini wanaweza wakatoka na jibu.
“Nikuhakikishie tu kwamba, mchakato wa usajili unaendelea na kamati husika inakutana wikiendi hii kupitia na kuangalia mahitaji ya benchi la ufundi na baadaye kila kitu kitawekwa wazi,” alisema.
Licha ya Katibu huyo kutoweka wazi majina ya wachezaji wanaoondoka, lakini DIMBA lilipata taarifa kutoka kwa mmoja wa vigogo wa Simba kwamba Mavugo na Mwanjali wapo kwenye mstari mwekundu.
Dirisha dogo la usajili wa wachezaji linafunguliwa rasmi Novemba 15, siku ya Alhamisi wiki ijayo.