Saturday, December 2, 2017

Mawingu Tz

Umeipata Hii? Joseph Omog Anataka Kutimua Wachezaji Hawa Dirisha Hili Dogo La Usajili

KOCHA Mkuu wa Simba, Joseph Omog, amewasili salama kule kwao Cameroon, lakini amempa rungu msaidizi wake, Masoud Djuma, kwamba mchezaji yeyote atakayezingua apigwe chini fasta, yaani akirejea asimkute Msimbazi.



Omog katika ripoti yake akishirikiana na Djuma walipendekeza asajiliwe beki wa kati mwenye uwezo wa kucheza pembeni, kipa, winga mwenye uwezo wa kucheza kushoto na kulia pamoja na straika mwenye uchu.

Amesisitiza kama Kamati ya Usajili ya Msimbazi itataka kusajili mchezaji yeyote raia wa kigeni, ni lazima mchezaji huyo afanyiwe majaribio kwanza ili kuona kama anafaa au hafai na wasifanye usajili tofauti na maagizo hayo.


“Kocha ameniambia niwasimamie na kuangalia kama wanaweza kufikia yale mahitaji ambayo tulikuwa tunataka wachezaji wa aina hiyo, kama kutakua na watakaoshindwa niachane nao,” alisema Djuma ambaye duru zinaonyesha kwamba anaandaliwa kuwa Kocha Mkuu Msimbazi.


Hiyo inamaanisha straika wa Rayon Sports, Shasir Nahimana, aliyewaambia Simba kuwa yeye si mchezaji wa kujaribiwa Msimbazi, basi moja kwa moja hatasajiliwa.

Mchezaji huyo alipendekezwa na Djuma, lakini wakala wake akaonyesha jeuri akidai kwamba kwa levo ya Simba, mteja wake ni mtu wa kusaini tu na kuanza kutiririsha mabao.


Simba wameshanza kupokea wachezaji wa kigeni kama Jonas Sakuwaha kutoka Zesco United ambaye alitua alfajiri ya Jumatano na beki wa kati Malik Ismaila kutoka Ghana. Hao watanza mazoezi na timu hiyo Jumatatu katika Uwanja wa Chuo cha Polisi Kurasini, jijini Dar es Salaam.


Omog amemuachia ujumbe msaidizi wake huyo ambaye yupo hapa nchini atakayesimamia mazoezi hayo na amempa rungu kamili kuwa kama kuna mchezaji ambaye atakuja kufanya majaribio na ataonekana anabahatisha, ampige chini.


Djuma pia atakuwa anasimamia mazoezi ya wachezaji wazawa waliobaki kutokana na wachezaji wa kigeni kupewa mapumziko ya siku 14 ambapo wengi wao watasafiri kwenda makwao.

Tupe Maoni Yako