Saturday, December 2, 2017

Mawingu Tz

Kakolanya Amnyoshea Mikono Kocha Wake Juma Ponda Mali.

Kipa wa Yanga, Beno Kakolanya amesema, kwa kipindi kifupi alichokaa na kocha wake, Juma Pondamali, amejifunza mengi na hata ikitokea ameachana na klabu hiyo, ana vingi vya kujivunia.
Beno ambaye kwa sasa yupo kwenye hali ya sintofahamu kama anaweza kuendelea na Yanga au akaachana nao kutokana na kudai sehemu ya pesa zake ya usajili, mesema mafunzo anayoyapata kutoka kwa Pondamali ambaye ndiyo anawanoa makipa wote wa Yanga ni ngumu kwa timu pinzani kuwafunga, hata kama mechi hiyo ina presha kubwa.
“Aisee, Pondamali ni bonge la kocha na vitu viwili ambavyo najivunia kutoka kwake ni namna ya kupanga timu inaposhambuliwa na namna ya kuwasiliana na wenzangu hasa beki. Timu inaposhambuliwa kuna namna unatakiwa kuipanga na ikishinda pia kuna upangaji wake, hilo linasaidia Yanga kuwa imara zaidi na kutoyumbishwa na wapinzani,”alisema Kakolanya ambaye ameshindwa kutamba mbele ya Mcameroon Youth Rostand.
Ameongeza na kuzungumzia changamoto ya nafasi ya kucheza alisema: “Siku nikikaa golini tu, ushindani utaanza upya, itabaki kuwa kazi ya kocha kumuachia nani ampange kwenye mechi ili apate matokeo mazuri.”
Kuhusu nafasi kwenye timu ya taifa alisema: “Majeruhi yaliyokuwa yananishumbua ndiyo tatizo, naamini wakiniona nacheza nitaitwa tu,ndio maana nimesema Yanga nikicheza ushindani utaanza upya,naendelea kujipanga na wala siwezi kukata tamaa.”
-Mwanaspoti

Tupe Maoni Yako