Kama ulisikia kwamba Messi, Mascherano, Ronaldo na Mourinho tayari walishaingia kwenye mzozo wa sheria za kule Hispania ambapo wote walipatikana na hatia juu ya kukwepa kulipia kodi!
Vipi kwa sasa?
Kwa sasa kesi kama hiyo imemkumba kiungo mshambuliaji wa Real Madrid aitwaye Luca Modric ambapo naye anadaiwa kufanya kosa hili! Hii ilikuwa ni mwaka 2014 na sasa mamlaka zinazohusu kodi za nchini humo zimeanza kumfanyia uchunguzi zaidi.
Hali inavyodaiwa kuwa
Inasemekana kwamba katikati ya mwaka 2013 na 2014 Modric alikwepa kulipa kiasi cha paundi 770,000 ambapo inadaiwa kuwa tukio hilo alilifanya akishirikiana na mke wake! Tungoje kuona namna itakavyokuwa.
Tupe Maoni Yako