Friday, December 22, 2017

Mawingu Tz

Donda Ndugu...Taifa Stars Yazidi Kuporomoka Viwango Vya FIFA

Tanzania imeporomoka kwa nafasi tano kwenye viwango vya shirikisho la soka duniani, FIFA kwa mwezi Novemba.
Taarifa iliyotolewa na FIFA leo inaonyesha Tanzania inashika nafasi ya 147 kutoka ya 142 mwezi Oktoba, wakati Uganda imeendelea kuongoza kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, ikiwa inashika nafasi ya 75 duniani – na Senegal inaendelea kuongoza kwa Afrika nzima ikiwa inashika nafasi ya 23 FIFA.
Katika 10 Bora mwezi huu Ujerumani bado inaongoza ikifuatiwa na Brazil, Ureno, Argentina, Ubelgiji, Hispania, Poland, Uswisi, Ufaransa na Chile.

Tupe Maoni Yako