Simba imevuliwa ubingwa wa Kombe la Shirikisho baada ya kufungwa kwa penalti 4-3 dhidi ya Green Worriors inashiriki Ligi Daraja la Pili.
Mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, iliisha kwa sare ya mabao 1-1 kwa dakika 90.
Baada ya hapo iliamualiwa kwa mikwaju ya penalti na wachezaji watatu wa Simba, Muzamiru Yassin, Hussein Zimbwe ’Tshabalala’ na Jonas Mkude walikosa penalti zao.
Kipa Aishi Manula wa Simba na Shabani Dihile walijipangua mikwaju ya penalti
Michuano ya Kombe la Shirikisho ya Azam Sports, imeendelea leo na timu kadhaa zimekutana na vipigo.
Matokeo mengine ya mechi za jana yako haya hapa…
Stand 3-0 AFC
Polisi Dar 5-0 Mgambo
Kariakoo Lindi 6-5 Transit Camp
Singida 2-0 Bodaboda
Biashara Mara 1-0 Mawenzi Market
Tupe Maoni Yako