Ni kipindi cha dirisha dogo la usajili kwa ligi mbalimbali za Tanzania bara kwa ajili ya timu kuboresha vikosi vyao kwa kusajili wachezaji wapya na kuacha au kuwatoa kwa mkopo wale ambao hawapati nafasi kwenye vikosi vya kwanza.
Afisa habari wa Simba, Haji Manara amesema kikosi chao ni lazima kifanye usajili katika kipindi hiki, Manara amesema tayari ripoti ya benchi la ufundi imeshafika kwa kamati ya usajili ambako wanamalizia mchakato wa nani asajiliwe kisha wapeleke kwenye kamati ya utendaji.
“Simba itaongeza mchezaji, tumeshapokea ripoti ya benchi la ufundi ipo kwenye kamati ya usajili na wao wapo kwenye kumalizia mchakato. Nadhani wiki ijayo kamati ya utendaji itaridhia bila shaka na tutatangaza nani anaingia.”
“Nani ataingia mimi sijui, lakini tutasajili bila shaka lazima tutaongeza mchezaji. Yanayoandikwa kwenye magazeti na mitandao ya kijamii ni tetesi. Tetesi kwenye kipindi cha usajili ni jambo la kawaida dunia nzima, mimi sina tatizo nalo.”
Tupe Maoni Yako