Soka ni mchezo ulio katika damu ya kila mtu, kila mmoja akiuona mpira anachanganyikiwa.
Hii ilitokea wiki iliyopita, Yanga wakiwa mazoezini kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Wakiwa ndiyo wanamalizia, mpira ulipigwa ukatoka nje na kuwakuta askari wa usalama barabarani wakiwa katika mazoezi yao ya kuendesha pikipiki kwenye sehemu ya kukimbilia uwanjani hapo.
Trafiki mmoja, aliupokea mpira huo kwa mbwembwe na kuanza kupiga kontroo kwa ustadi mkubwa kabla ya kuachia pasi saaafi na kuwashangaza wengi waliokuwa eneo hilo.
Tupe Maoni Yako