KAMA Yanga watakuwa wamedhamiria kumletamshambuliaji wa Nkana Rangers, Walter Bwalya nchini, watapaswa kuvunja benki na kutoa dau la Sh milioni 300, ambazo zinatakiwa na klabu hiyo ya Zambia.
Bwalya amekuwa akitajwa sana na klabu kubwa nchini, lakini kwa upande wa Simba na Azam FC, zimeonekana kuachana na mshambuliaji huyo na kuwaacha Yanga kuendelea kuwinda saini ya mchezaji huyo.
Lakini huenda Yanga wakawa na kazi ngumu kuhakikisha wananasa saini ya Bwalya, baada Nkana Rangers kuweka wazi kwamba hawatashusha dau lao wanalotaka la Sh milioni 300.
Akizungumza na BINGWA, Katibu Mkuu wa Nkana, Ken Mwansa, alisema hawawezi kumzuia mchezaji huyo kwenda katika timu inayomhitaji, ila wanachoangalia ni timu hiyo kuwa tayari kuvunja mkataba wa mchezaji huyo.
Alisema wanahitaji timu inayomhitaji mchezaji huyo aliyebakiza mkataba wa mwaka mmoja kupeleka barua ya maombi kwa uongozi, ambapo wao wako tayari kumuuza.
“Tupo tayari kumuuza Bwalya kwa timu yoyote inayomhitaji, lakini klabu hiyo lazima ije tuzungumze na dau lake halitakuwa tofauti na lile tulilowatajia Azam FC, ambalo ni shilingi milioni 300,” alisema Ken.
-Bingwa
Tupe Maoni Yako