Sunday, December 3, 2017

Mawingu Tz

Taarifa Mpya Kutoka Yanga Kuhusu Hali Ya Kamusoko

Matumaini kuwa kiungo Thabani Kamusoko atapona haraka na kurejea uwanjani yamepaa baada ya kuonekana akipata matibabu ya vipimo vya juu.

Kabla, Kamusoko raia wa Zimbabwe alikuwa akitibiwa bila ya kuchukuliwa vipimo hivyo, hali iliyomsababisha kukaa nje kwa muda mrefu.

Kuanzia juzi, Kamusoko ameanza kupata matibabu ya kina zaidi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Mmoja wa madaktari wa michezo nchini ambaye hakupenda jina lake liandikwe amesema kupitia vipimo anavyofanyiwa, ni uhakika wa kupata matibabu bora.

“Unajua kipimo kile hakiongopi, ukitoka pale lazima utajua tatizo lako ni nini. Maana yake, daktari atajua akusaidiaje.

“Unajua daktari anategemea majibu ya vipimo ndiyo akusaidie. Sasa inawezekana kabla hawakuwa wakimchukua vipimo sahihi,” alisema.


“Lakini pale unaweza kusema atajua tatizo na rahisi kulifanyia kazi, akimaliza matibabu atarejea uwanjani.”

Tupe Maoni Yako