Bilionea Mohammed Dewji, amepita katika mchakato wa uwekezaji wa klabu ya Simba na ofa yake ya Sh bilioni 20. Lakini mwenyekiti wa kamati ya utoaji zabuni iliyokuwa imeundwa amesema ilikuwa kazi ngumu kwao.
Dewji amejitokeza na kuwa muwekezaji pekee ambaye aliweka dau la Sh bilioni 20 kupata hisa asilimia 51.
Jaji mstaafu Thomas Mihayo amesema ilikuwa kazi ngumu kwa muwa Mo Dewji alikuwa mtu pekee aliyekuwa amepeleka maombi.
“Kweli kulikuwa na ugumu sana, halikuwa jambo rahisi kwa kuwa hata sisi hatukupenda. Maana alikuwa ni mtu mmoja tu aliyeomba,” alisema.
“Hii ikatufanya tupitie kwa umakini zaidi. Lakini mwisho ndiyo imekuwa hivyo Mo Dewji amepita na kitachofuatia ni majadiliano mengine baada ya mkutano wa leo,” alisisitiza.
Wanachama wa Simba walijitokeza kwa wingi katika mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Tupe Maoni Yako