Baada ya kuwepo na taarifa kuwa Klabu ya Simba ipo katika mipango ya kumuwania beki wa kati Asante Kwasi raia wa Ghana anayeoichezea Lipuli, kuna taarifa mpya kuhusu mchakato huo.
Siku kadhaa za nyuma ilielezwa kuwa beki huyo ambaye msimu uliopita alikuwa akiichezea Mbao FC ya jijini Mwanza alishaanza kuzungumza na upande wa Simba kuhusu usajili wake.
Selemani Matola ambaye ni kocha wa mchezaji huyo katika kikosi cha Lipuli FC amesema bado hawajapata ofa yoyote kutoka Simba na hivyo hajui chochote kuhusu mchakato huo.
Matola ambaye ni kiungo wa zamani wa Simba na timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, amesema kuwa wao wapo kwenye mikakati ya kufanya usajili wachezaji wapya na Kwasi ni mchezaji ambaye bado yupo kwenye mipango yake.
Tupe Maoni Yako