Friday, December 8, 2017

Mawingu Tz

Simba Waona Isiwe Tabu...Waamua Kumtumia Juuko Wajumbe

Kutokana na beki wake, Juuko Murshid kuonekana ni lulu na kuzivutia timu kadhaa wakiwemo watani wao Yanga, Simba wameanza kujipanga.

Taarifa zinaeleza, Simba imeamua kumtuma mjumbe kwenda Kenya ambako Juuko anaitumikia timu yake ya taifa ya Uganda katika michuano ya Chalenji.


"Lengo ni kuzungumza naye mambo kadhaa na kumueleza msimamo wa Simba. Unajua mengi yanazungumzwa na huenda yakasababisha aelewe tofauti," kilieleza chanzo.

"Siku zinakwenda na Juuko anajua kwamba Simba bado inamhitaji lakini si vibaya kukutana naye na kuzungumza naye."

Yanga ni kati ya timu zilizoonyesha nia ya kuimarisha safu yake ya ulinzi kwa kumnasa Mganda huyo.

Tupe Maoni Yako