Wakati akiendelea kusubiri hatma yake ndani ya kikosi cha Yanga, mshambuliaji raia wa Zimbabwe Donald Ngoma ameendelea kujifua kivyake.
Ngoma alizuiwa kufanya mazoezi na kikosi cha Yanga na uongozi mpaka pale Kamati ya Utendaji itakapotoa maamuzi kuhusu kesi yake.
Ngoma anatuhumiwa kuondoka kambini kwenda kwao Zimbabwe bila ya ruhusa ya uongozi.
Tayari amewasilisha utetezi wake vikiwemo vielelezo vya matibabu kwa Kamati ya Utendaji ya Yanga.
Tupe Maoni Yako