Tuesday, December 12, 2017

Mawingu Tz

Jezi Ya Kwasi Mazoezini Yawachanganya Mashabiki, Wasema Amemalizana Na Simba

Beki nyota wa Lipuli ya Iringa, Asante Kwasi amewachanganya mashabiki wa Simba baada ya kuonekana akiwa na jezi nyekundu akijifua gym.

Baada ya picha hiyo, wengi wameanza mjadala wakiamini Kwasi amemalizana na Simba, lakini taarifa zinaeleza kweli wako katika hatua za mwisho.

Hata hivyo, jezi aliyovaa Kwasi ni jezi ya mazoezi ya Lipuli ya Iringa kwa kuwa nayo inatumia rangi nyekundu na nyeupe na si Simba kama ambavyo wengi wameonekana kuamini.

Kwasi bado yuko kwao nchini Ghana kwa mapumziko na amekuwa akiendelea na mazoezi kwa juhudi kubwa.


Lakini Simba ilishaonyesha nia ya kumnasa Kwasi wakati huu wa dirisha dogo la usajili.

Tupe Maoni Yako