Timu inayowania kumtwaa Said Hamis Ndemla, imeteremka daraja nchini Sweden.
Timu ya AFC imeteremka daraja baada ya kushindwa kufanya vizuri katika mechi zake mbili za mwisho, wiki iliyopita.
Wakati Ndemla amefuzu majaribio na timu hiyo imeonyesha nia ya kumtwaa. Maana yake, kama atafanikiwa kujiunga nayo atakuwa na kazi ya kuisaidia kurejea Ligi Kuu Sweden baada ya kuwa imeteremka hadi daraja la kwanza.
Uongozi wa AFC, ulilazimika kumfukuza kocha wake, Pere Olson ambaye aliwahi kuwa kocha wa Haruna Moshi ‘Boban’ wakati akikipiga Sweden.
Olson alishindwa kuliongoza jahazi la AFC ambayo pia anaichezea Thomas Ulimwengu ambaye sasa ni majeruhi.
Tupe Maoni Yako