Sunday, December 10, 2017

Mawingu Tz

Z’bar Heroes yahofiwa kutumia Njia Za Panya Kupata Ushindi

Kiwango kinachooneshwa na Zanzibar Heroes kwenye michuano ya kombe la Chalenji kimeendelea kushtuwa wengi, kubwa kuliko ni leo Dec. 9, 2017 baada ya mchezo dhidi ya wenyeji Kenya, baadhi ya wachezaji wa Zanzibar Heroes walitakiwa kupimwa wakishukiwa kutumia dawa za kusisimua misuli ambazo zimezuliwa kwenye michezo.
Mchezo huo ulimalizika kwa suluhu (Kenya 0-0 Zanzibar Heroes) lakini maafisa wa CECAFA waliwataka baadhi ya wachezaji wachukuliwe vipimo kwa ajili ya kufaniwa uchunguzi kama wanajihusisha na matumizi ya dawa zilizozuiliwa michezoni.
Baadae maafisa wa CECAFA wakiwa wameongozana na madaktari walifika hotel waliyofikia wachezaji wa Heroes (Garden Hotel) kisha kuchukua vipimo kwa wachezaji wanne.
Wachezaji waliochukuliwa vipimo ni Fesal Salum, IbrahimHamad, Suleiman Kassim ‘Selembe’, na Mohamed Issa ‘Banka’. Watatu kati ya wachezaji wameshinda tuzo ya man of the match katika mechi tatu tofauti (Mohamed Issa-Zanzibar vs Rwanda, Ibrahim Hamad-Tanzania vs Zanziba na Fesal Salum-Kenya vs Zanzibar)

Tupe Maoni Yako