Mwaka 2005 ilikuwa mara ya mwisho kwa klabu ya Manchester United kucheza mchezo wa michuano ya FA halafu mchezo huo usioneshwe, na kuanzi kipindi hicho hadi sasa United wamekuwa wakioneshwa mechi zao za FA.
Mchezo ambao United haukuoneshwa ulikuwa mchezo wao wa nyumbani wakati wakiikaribisha Exeter City ulioisha bila bila lakini sasa mchezo wao ujao vs Derby Country nao hautaoneshwa katika Tv.
Kampuni za BBC na Bt Sports ambayo ndio yanarusha matangazo yao hayajauchagua mchezo kati ya Manchester United na Derby Country kuwa kwenye orodha ya michezo itakayooneshwa, jambo ambalo limewashtua wengi.
Michezo ya timi zote kubwa zilizobaki itaoneshwa ikiwemo mchezo wa kwanza January 5 kati ya Liverpool vs Everton huku pia mchezo kati ya mabingwa watetezi Arsenal vs Nortigham Forest nao utaoneshwa BT Sports.
Tupe Maoni Yako