Benchi la ufundi la klabu ya Yanga limetoa Mapumziko ya wiki moja kwa wachezaji wake ambao hawakuitwa kwenye timu za Taifa ile ya Bara Kilimanjaro Stars na ile ya Zanzibar Zanzibar Heroes.
Dismas Ten ameiambia Chandimu kuwa baada ya wiki moja timu itaendelea na utaratibu wa mazoezi kujiandaa na mechi zilizosalia za mzunguko wa Kwanza wa Ligi Kuu soka ya Tanzania Bara VPL 2017/2018.
USAJILI DIRISHA DOGO
Dismas Ten amesema pia tayari wamekamilisha usajili wa Nyota wawili Fiston Kayembe aliyetoka nchini Congo na anacheza nafasi ya Ulinzi kama beki wa kati na pia wamemsaini Yohanna Mkomola ambaye alikuwa mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 17 Serengeti Heroes.
Tupe Maoni Yako