Saturday, December 2, 2017

Mawingu Tz

CAF Yamwaga Mpunga Mrefu Kwa Nchi Za Afrika Zilizofuzu Kombe La Dunia…Yaweka Matumaini Makubwa


Shirikisho la Vyama vya Soka Afrika (CAF) limetoa ruzuku ya Dola 500000 kwa kila timu ya Afrika iliyofuzu Kombe la Dunia ili ziwasaidie katika maandalizi yao ya kujiandaa na fainali hizo zitakazofanyika mwakani nchini Russia
Kiasi hicho ambacho ni zaidi ya Shilingi 1.1bilioni kitagawanywa kwa timu za Morocco, Misri, Nigeria, Senegal na Tunisia ambazo zinakwenda kupeperusha bendera ya Afrika katika fainali hizo za mwakani.
Kwa kujibu wa taarifa iliyotolewa na CAF, uamuzi wa kuzipa fedha na msaada mwingine timu hizo umetokana na maadhimio ambayo kamati ya utendaji ya CAF iliyaweka Novemba 16 chini ya Makamu wa Rais, Kwesi Nyantaky kutaka timu za Afrika zifanye vema kwenye fainali hizo.
Mafanikio makubwa ya Afrika katika Kombe la Dunia ni kucheza hatua ya 16 bora iliyofikiwa na Cameroon (1990), Senegal (2002) na Ghana (2010).

Tupe Maoni Yako