Saturday, December 9, 2017

Mawingu Tz

Beki Kisiki Akatiza Likizo Yake Eti Kisa Chirwa Na Okwi

Beki wa Kati wa Mwadui FC, Idd Mobby “Kiraka” amesema kutokana na kasi ya washambuliaji wa Ligi Kuu ameamua kutopumzika na kueendelea kujifua kivyake.
Washambuliaji wa Ligi Kuu tishio msimu huu ni Ibrahim Ajib, Obrey Chirwa(Yanga), Emmanuel Okwi (Simba), Mohamed Rashid (Prison), Habib Kiyombo (Mbao FC) na Mbaraka Yusuph wa Azam.
Ligi Kuu sasa imesimama kupisha Mashindano ya Chalenji inayoendelea nchini Kenya huku timu mbalimbali zikiwapa mapumziko wachezaji wao.
Kiraka alisema msimu huu washambuliaji wamekuwa na kasi kubwa uwanjani jambo linalofanya ajifue zaidi ili kuwa fiti kupambana nao.
Alisema licha ya kupewa mapumziko na uongozi wa timu hiyo, lakini kwake ameendelea kufanya mazoezi ambayo amesema akirejea awe fiti zaidi.
“Nipo Shinyanga kwa sasa na nimeamua nisipumzike bali niendelee kujifua mazoezini mana hawa washambuliaji msimu huu wamekuwa na kasi ya ajabu ukiwa una mazoezi basi utakuwa uchochoro”alisema Kiraka.
Beki huyo alisema kwa ujumla Ligi Kuu msimu huu imeanza kwa ushindani mkubwa na hilo limetokana na klabu kufanya maandalizi makini haswa kwenye usajili.
“Ligi Kuu ni ngumu angalia sasa kila mchezo unakuwa na upinzani mkubwa si nyumbani wala ugenini.”

Tupe Maoni Yako