Saturday, December 9, 2017

Mawingu Tz

Kumbe Simba Na Yanga Ndo Tatzo Kilimanjaro Stars Aisee


Licha ya kupata matokeo yasiyoridhisha katika mashindano ya Kombe la Chalenji, kwa Kilimanjaro Stars wadau wa soka jijini Mwanza wamesema bado nafasi ipo kwa timu hiyo kusonga mbele.
Kilimanjaro Stars ipo nafasi ya nne kwenye kundi lao A, ikiwa na pointi moja baada ya kushuka uwanjani mara mbili, huku ndugu zao Zanzibar Heroes wakiwa kileleni kwa alama sita.
Wakizungumza na mtandao huu baadhi ya makocha walisema bado Kilimanjaro ina nafasi endapo itashinda mechi mbili zilizobaki, huku ikiziombea mabaya timu pinzani.
Kocha John Tegete alisema kuwa Kilimanjaro inaweza kupenya, lakini iwapo timu za Zanzibar Heroes, Kenya na Libya zikipoteza mechi zao za mwisho.
Kocha alisema kilichoiponza timu hiyo hadi kuwa kwenye wakati mgumu ni washauri wa benchi la ufundi kwa kuwachagua wachezaji wengi wa Simba na Yanga.
“Bado nafasi ipo kama makosa waliyoyafanya yatarekebishwa, lakini washauri wa benchi la ufundi ndio wa kulaumiwa..kila siku wachezaji wale wale.”
“Lazima tuangalie wachezaji wengine, vijana wapo wengi hapa nchini ambao wanaweza kucheza mpira, siyo kila siku wachezaji wa Simba na Yanga,” alisisitiza Tegete.
Naye Omary Bakari alisema mpira ni mchezo wa wazi, ambao unaweza kubadilika dakika za mwisho, hivyo bado matumaini yapo kwa Kili Star.
“Mimi kama mdau naona bado nafasi ipo kwa timu yetu, ni suala la benchi la ufundi kuhakikisha kasoro zote zinafanyiwa kazi ili kushinda mechi zilizobaki,” alisema Bakari.

Tupe Maoni Yako