Wednesday, December 20, 2017

Mawingu Tz

Ujumbe Aliotoa Nduda Unatishia Maisha Ya Manula Simba


KIPA namba mbili wa Simba, Said Mohamed ‘Nduda,’ ameanza rasmi mazoezi huku akitamka wazi kuwa malengo yake ni kuwa kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo.
Kauli hiyo ni kama anatuma ujumbe kwa kipa mwenzake Aishi Manula, ambaye ndiye amekuwa chaguo la kwanza la kikosi hicho.
Nduda amekuwa majeruhi kwa zaidi ya miezi miwili na Simba ilimpeleka kutibiwa nchini India, ambako alifanyiwa upasuaji wa goti.
Kipa huyo hajagusa mchezo wowote wa Ligi Kuu msimu huu kutokana na majeraha hayo, lakini sasa ameanza mazoezi ya gym katika Chuo cha Polisi, Kurasini.
Kipa huyo amesema  kwamba, ana siku tatu tangu ameanza mazoezi ya Gym chini ya uangalizi wa daktari wa timu hiyo, Yassin Gembe na atafanya kwa muda wa wiki mbili kabla ya kurejea uwanjani.
“Wameniambia Gym ni wiki mbili hadi leo (jana) ni siku yangu ya tatu, hivyo baada ya muda huu nadhani nitamsikiliza daktari kwa ajili ya kunipangia programu nyingine ikiwamo ya mazoezi ya uwanjani.
“Nadhani nikirejea nitahakikisha napambana kwani kila mmoja anataka kuwa kikosi cha kwanza, inaniuma sana natamani nipone haraka niweze kuendelea na majukumu yangu ya klabu kuhakikisha tunapambana kufikia malengo yetu ya kushinda kila mechi hasa kutwaa mataji,” alisema Nduda.


Tupe Maoni Yako