Friday, December 29, 2017

Mawingu Tz

Mwinyi Aandika Barua Yanga Akitaka Aachwe, Afc Leopard Ya Kenya Ndiyo Chanzo


Beki wa kushoto wa Yanga, Mwinyi Haji ameiandikia barua klabu yake akitaka imuachie aende zake kutafuta maisha.


Haji ameindika barua akitaka Yanga imuachie aende kujiunga na klabu ya AFC Leopards ya Kenya ambayo tayari kumsajili.

Akizungumza na SALEHJEMBE, Haji amesema ameona hana nafasi ya kucheza katika kikosi cha Yanga, hivyo angependa kwenda kujiendeleza zaidi.

"Kama sina nafasi, maana yake sina msaada na sihitajiki. Hivyo kwa makubaliano mazuri bila ya kugombana acha niende nikajiendeleze.

"Kazi yangu ni soka na ninataka kujiendeleza. Siwezi kuendelea nikiwa benchi, hivyo Yanga nimewaandikia waniachie niwahi kujiunga na AFC Leopards," alisema.

Beki huyo alionyesha kiwango cha juu na kuisaidia Zanzibar Heroes kufika fainali ya Kombe la Chalenji lililomalizika wiki moja na ushee iliyopita.

Tupe Maoni Yako