Showing posts with label AZAM. Show all posts
Showing posts with label AZAM. Show all posts

Wednesday, December 27, 2017

Mawingu Tz

Himid Mao huyooo Yanga

SASA ni rasmi kuwa kiungo wa Azam, Himid Mao ‘Ninja’, anaweza kutua Yanga iliyokuwa ikimsaka kwa muda mrefu baada ya mchezaji huyo kushindwana na timu aliyokwenda kujiunga nayo ya Bidvest West ya Afrika Kusini.
Yanga ilikuwa ikimwania Mao tangu msimu uliopita, ikimwona kama suluhisho katika nafasi ya kiungo mkabaji.
Baada ya kumkosa, ilipiga hodi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na kumtwaa Papy Tshishimbi aliyeonyesha kiwango cha hali ya juu na kuwa kipenzi cha mashabiki wa Wanajangwani hao.
Moja ya sababu iliyowafanya Yanga kumkosa Mao, ni mpango wa kiungo huyo kwenda kucheza soka la kulipwa Afrika Kusini.
Lakini habari zilizopatikana jijini Dar es Salaam jana, zinasema kuwa Mao ameshindwana dau na Bidvest West na hivyo amerejea nchini kuendelea na maisha yake ndani ya Azam.
Kwa hali hiyo, iwapo Yanga wataendelea kumuhitaji, wanaweza kumtwaa mwishoni mwa msimu.
Chanzo cha kuaminika cha BINGWA kutoka ndani ya Azam, kinasema: “Kuna asilimia 75 za Himid Mao kubaki Azam kwani alipokwenda ‘South’ (Afrika Kusini) kwenye mazungumzo na klabu ya Bidvest, walishindwana katika suala la ‘mtonyo’ (fedha), hivyo msimu huu atabaki Azam, msimu ukimalizika anaweza kwenda timu nyingine lakini si Bidvest West tena.”
BINGWA lilimtafuta Mao kuzungumzia hilo ambapo alisema: “Nikweli nilikuwa Afrika Kusini, lakini siwezi kutaja ni klabu gani, pia sikuwa nimekwenda kwa lengo la kufanya majaribio kwani majaribio nilishafanya muda mrefu, nilienda kwa ajili ya mazungumzo na yamekwenda vizuri.”
Mao ni miongoni mwa viungo hodari wakabaji hapa nchini akiwa pia ni nahodha na tegemeo la timu ya Taifa, Taifa Stars.

Friday, December 22, 2017

Mawingu Tz

Yanga Yaikimbiza Simba Viwango Vya Ubora Afrika, Fifa

Unaweza ukabisha ila ndiyo ukweli. Klabu ya Yanga inaongoza kwenye viwango vya ubora vya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) dhidi ya watani zao Simba baada ya viwango vya ubora kuonyesha inashika nafasi ya 345 kwa ubora Afrika baada ya mechi zilizochezwa Desemba 17.
Wapinzani wao Simba wanashika nafasi ya 371 huku Azam nao wakiwa nafasi ya 365 kwenye viwango hivyo. Taarifa ya viwango hivyo inayopatikana kwenye mtandao wa footballdata base.com ilioshesha klabu ya Esperance de ndiyo inashika nafasi ya kwanza barani Afrika.

Wednesday, December 20, 2017

Mawingu Tz

Azam Fc Yapata Pigo….Kumpeleka Mbaraka Yusuf Afrika Kusini

Mshambuliaji Mbaraka Yusuf wa Azam FC atakwenda kupata matibabu nje ya nchi.

Msemaji wa Azam FC, Jaffar Iddi amesema uongozi wa klabu hiyo, baada ya kupata majibu ya vipimo vyake, kesho ataondoka nchini kwenda Afrika Kusini.

“Majibu yanaonyesha ameumia meniscus kama ambavyo nilieleza awali. Hivyo atakwenda Afrika Kusini kesho kwa ajili ya matibabu,” alisema.


Mbaraka aliumia wakati akiitumikia timu ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars wakati akiitumikia katika michuano ya Chalenji.

Awali kulikuwa na taarifa kwamba Azam FC ilimtelekeza, jambo ambalo baadaye lilikanushwa na klabu ya Azam FC kwamba imekuwa ikiendelea kufuatilia hali yake.

Tuesday, December 19, 2017

Mawingu Tz

Azam Fc Yaweka Sawa Kuhusiana Na Mbaraka Yusuf Kuumia Timu Ya Taifa





Klabu ya Azam FC imesema mshambuliaji wao, Mbaraka Yusuf amegundulika ana tatizo la mfupa laini wa goti.

Msemaji wa Azam FC, Jaffar Iddi Maganga amesema, Mbaraka amegundulika ana tatizo hilo la Meniscus baada ya kufanyiwa vipimo akiongozwa na daktari wa klabu hiyo, Juma Mwankemwa.

“Kwa hiyo matibabu yanaendelea na klabu ya Azam FC ndiyo inayoshughulikia, hivyo suala la kwamba ametelekezwa, hapana,” alisema.


Mbaraka aliumia wakati akiitumikia timu ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars katika michuano ya Chalenji iliyomalizika kwa wenyeji Kenya kubeba kombe dhidi ta Zanzibar Heroes kutoka Tanzania.

Wednesday, December 13, 2017

Mawingu Tz

Himid Mao Mbioni Kumalizana Na Timu Hii Ya Afrika Kusini

Wakati dirisha dogo la usajili likielekea kufungwa siku chache zijazo, kuna taarifa kadhaa kuhusu usajili wa wachezaji wa Tanzania.
Inadaiwa kuwa kiungo mkabaji wa Azam FC, Himid Mao, amefuzu majaribio ya kujiunga na Klabu ya Bidvest inayoshiriki Ligi kuu ya nchini Afrika Kusini na yuko mbio kwenda kumalizana naoHimid Mao – Tanzania.
Bado hakuna taarifa kamili kutoka Azam FC juu ya taarifa hizo za usajili.
Aidha, upande mwingine inaelezwa kuwa Muhsin Makame ambaye ni mshambuliaji wa Serengeti Boys amejiunga na Njombe Mji kwa mkopo akitokea Klabu ya Mtibwa Sugar ya mkoani Morogoro.

Tuesday, December 12, 2017

Mawingu Tz

Madrid Waanza Tamaa Kwa Salah, Yataka Kutoa Fedha Na Mchezaji Impate


Mavituuuz ya Mohamed Salah yanaonekana kuwachanganya matajiri Real Madrid ambao wameweka hadharani kwamba wanamtaka.

Tayari Salah aria wa Misri na mchezaji bora wa BBC, amefunga mabao 18 katika mechi za Ligi Kuu England na Ligi ya Mabingwa Ulaya.


Imeelezwa tayari thamani ya Salah aliyetokea AS Roma imefikia pauni million 39 na Madrid inaonekana inataka kumtwaa na pamoja na kuilipa Liverpool, itamtoa Lukas Vazquez.

Salah anaonekana kuwa ndiyo tegemeo la Liverpool katika ushambulizi kila siku zinavyosonga mbele.

Raia huyo wa Misri amekuwa tegemeo katika uchezaji wa timu, utoaji wa pasi za mabao na wakati mwingine kufunga mwenyewe.