Wednesday, December 6, 2017

Mawingu Tz

USAJILI YANGA:Hawa Hapa Wachezaji Wanaoondoka Yanga Kwenye Dirisha Hili Dogo La Usajili


Kocha mkuu wa Yanga, Mzambia, George Lwandamina amemruhusu straika wake, Matheo Anthony kuondoka klabuni hapo ili akatazame maisha sehemu nyingine baada ya kuona hatakuwa na nafasi ya kumtumia tena msimu ujao.

Matheo ambaye alijiunga na Yanga misimu mitatu nyuma akitokea KMKM ya Zanzibar hana nafasi yake ya kucheza kwenye kikosi cha timu hiyo kutokana na wingi wa washambuliaji.
Kwa sasa kuna uwezekano mshambuliaji huyo akatimkia Lipuli FC ya Iringa kutokana na klabu hiyo kuonyesha nia ya kumhitaji.
Chanzo makini kimesema kuwa ombi la Matheo limekubaliwa hivyo msimu huu hatokuwepo tena Yanga hadi pale mambo yatakapomnyokea huko aendako endapo atafanya vizuri kiasi cha kumshawishi tena kocha kumrudisha kikosini hapo.


“Lwandamina amemruhusu Matheo kuondoka na wenzake wengine watano ambao ni  Yusuf Mhilu, Baruan Akilimali, Juma Mahadhi, Maka Edward na Saidi Makapu, kocha kaona awaruhusu wote ili aweze kuangalia safu nyingine itakayokuwa na uwezo wa kutumika tofauti na ilivyosasa ambapo wengine wanaonekana kushindwa kumudu kasi yake,” kilisema chanzo hicho.

Tupe Maoni Yako