Tuesday, November 28, 2017

Mawingu Tz

Waliojua Lukaku Ataikosa Arsenal, Haya Ndiyo Maamuzi Ya FA



Straika wa Manchester United, Romelu Lukaku hatatumikia adhabu kwa kumchezea vibaya beki wa Brighton and Hove Albion Gaetan Bong Jumamosi.

Chama cha Soka cha England (FA) kimeamua kutochukua hatua zaidi dhidi ya mshambuliaji huyo kwa kushiriki kwenye tukio hilo dhidi ya Bong.

Sekunde chache kabla ya Lewis Dunk kujifunga na kuipa United goli la kuongoza katika ushindi wa 1-0 Old Trafford, Lukaku alionekana akimpiga teke Bong baada ya kushindana ndani ya eneo la penalti.

Ripoti zilidai kuwa Lukaku angefungiwa kuichezea United mechi tatu zijazo, ambazo zingekuwa ni pamoja na mechi dhidi ya Arsenal na Manchester City.

Inaelewa kuwa Lukaku hataadhibiwa tena na FA kutokana na tukio hilo baada ya kuchunguzwa zaidi na waamuzi wawili wa mechi.

Kama ilivyo, Lukaku yupo huru kucheza mechi yake ya 200 Ligi Kuu YA England katika Vicarage Road.

Lukaku amefunga mabao 12 akiwa United katika michuano yote tangu alipotua klabuni hapo akitokea Everton kwa pauni 75m, mechi ya wikiendi ijayo Man united itakipiga dhidi ya Arsenal kisha Man City.



Tupe Maoni Yako