Sunday, December 10, 2017

Mawingu Tz

Tetesi Za Usajili Barani Ulaya..Asensio Anukia Man Utd




Manchester United itafanya mchakato kumsajili kiungo wa Real Madrid Marco Asensio dirisha la uhamisho la Januari baada ya kuachana na mpango wa kumsajili Gareth Bale, kwa mujibu wa Don Balon.



Mashetani Wekundu wanajiamini watafanikiwa kumsajili mchezaji huyo wa miaka 21 kwani ameshindwa kupata nafasi ya kudumu Santiago Bernabeu.

MAN UTD KUMUUZA SHAW & DARMIAN


Manchester United wapo tayari kusikiliza ofa kuwauza mabeki wao Luke Shaw na Matteo Darmian, kwa mujibu wa The Daily Record.
Shaw ambaye amesumbuliwa na majeraha amepewa nafasi kujiunga na klabu nyingi za Uingereza wakati Muitaliano Darmian hatakiwi kwenye kikosi cha Jose Mourinho.

United wanataka kutunisha mfuko wao ili kuwasajili beki wa kushoto Alex Sandro na Danny Rose majira ya baridi.
BETIS WANATAKA KUMSAJILI STURRIDGE



Real Betis wanaandaa ofa kumsajili Daniel Sturridge kutoka Liverpool, kwa mujibu wa El Gol Digital .

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza amekuwa akihaha kutafuta muda wa kucheza zaidi Anfield na atapewa nafasi kutimkia Hispania Januari.
CHELSEA YAMTENGEA £20M BAILEY


Chelsea wapo tayari kutoa kitita cha paundi milioni 20 kwa ajili ya winga wa Bayer Leverkusen Leon Bailey, limedai The Sun .

Blues wamekuwa wakimfuatilia Mjamaica huyo kwa kipindi cha miezi 18 na wanataka kuipiku Barcelona kumsajili mchezaji huyo wa miaka 20.
MAN UTD WANATAKA KUMSAJILI ALEX SANDRO


Jose Mourinho amemfanya Alex Sandro wa Juventus kuwa shabaha nambari moja kutua Manchester United kucheza nafasi ya beki wa kushoto kwa mujibu wa Daily Record.

Tupe Maoni Yako