Tuesday, January 2, 2018

Mawingu Tz

Obrey Chirwa Mbioni Kutua Simba

Ni Kauli ambayo unaweza ukaisema kutokana na Hali iliyopo kwasasa kati ya Yanga na Straika wao kutoka nchini Zambia Obrey Chirwa.
Kulingana na Gazeti la dimba la Leo limeeleza kuwa Obrey Chirwa huenda akatua Msimbazi timu ya Simba endapo tu Yanga watashindwa kumtimizia mahitaji yake anayoyata kwasasa.
ISHU YA KUWADAI YANGA
Inadaiwa kuwa Yanga bado wanadaiwa na Obrey Chirwa ambaye kwa msimu huu amekuwa mchezaji muhimu sana upande wa Ushambuliaji kiasi cha Kugeuka kuwa Tegemezi eneo la Ushambuliaji.
Inadaiwa Chirwa ambaye alitarajiwa kutua Nchini siku ya Jumamosi kuja kwake Tanzania hakuja kwaajili tu ya Kucheza bali kufanya mazungumzo juu ya hatma ya madai yake.
MKATABA WAKE YANGA WAELEKEA MWISHONI
Mkataba kati ya Chirwa na Yanga  unaelezwa kuwa Uko mbioni kuisha kwani utaisha mwishoni mwa Msimu huu wa Ligi hivyo basi imesalia chini ya miezi 6 hivyo Upande wa Pili wa Simba unaotajwa kutoa Udenda Juu yake huenda ikawa rahisi kuanza kufanya naye maongezi mapema ili kumsajili kwaajili ya michuano ya kitaifa na Kimataifa.
ANATAKA DAU KUBWA ILI AONGEZE MKATABA YANGA
Taarifa za Ndani kutoka Yanga  zinadai Kuwa Chirwa anataka alipwe Shilingi milioni 120 ili Kuongeza Mkataba Yanga kutokana na kuongezeka kiwango chake msimu huu, Wakati hali ya Uchumi ndani ya Yanga inaelezwa kuwa siyo nzuri sana
YANGA NAO HAWATAKI MCHEZO KWENYE HILI
Klabu ya Yanga kwa upande wao inasemekana wapo katika mipango ya kuhakikisha wanamalizana na Chirwa mapema kabla hata muda wake haujaisha wa mkataba ili yasije kuwakuta kama yaliyowakuta kwa Niyonzima.
Hivyo wanasubiri waweke mambo sawa kisha wakae mezani na Chirwa ili kuangalia uwezekano wa Chirwa kuongeza makataba mapema.


Tupe Maoni Yako