Saturday, December 9, 2017

Mawingu Tz

USAILI:Mzamiru Yassin Aipa Yanga Siku 10 Tu

KIUNGO mkali wa mabao Ligi Kuu Bara, Mzamiru Yassin ameipa klabu ya Yanga siku 10 baada ya kuwaambia wasubiri kwanza amalizane na Michuano ya Kombe la Chalenji ndipo waanze kuzungumza kuhusu masuala ya usajili.
Kiungo huyo aliyeifungia Simba mabao 12 katika kipindi cha miezi 18 iliyopita, ametaka asihusishwe kwanza na suala lolote la usajili kwani mzigo wa kuisaidia Kilimanjaro Stars katika mashindano hayo ya Chalenji umekuwa mkubwa.
Habari kutoka kwa swahiba mkubwa wa Mzamiru, zinasema viongozi wa Simba, wana presha kubwa ya kumpoteza kiungo huyo na tayari wamemtuliza wakimwambia tayari timu hiyo imetua kwenye mikono ya bilionea Mohammed Dewji na maisha yatakuwa mazuri. Yanga inamhitaji Mzamiru kwa udi na uvumba ili akazibe nafasi ya Mzimbabwe, Thabani Kamusoko ambaye ameanza kuandamwa na majeraha ya mara kwa mara. Mzamiru amebakisha miezi sita katika mkataba wake na Simba, na kikanuni anaruhusiwa kuanza mazungumzo na timu yoyote mpya.
“Anaona kama ni habari zinazomchanganya, ameomba amalize kwanza majukumu ya kuitumikia timu yake ya Kilimanjaro Stars ndipo waanze kuzungumzia masuala hayo,” alisema swahiba.
Alipoulizwa Mzamiru mwenyewe, Alijibu kwa kifupi “Naomba tuzungumze kuhusu Chalenji, bado nina mkataba na Simba.”
-Mwanaspoti

Tupe Maoni Yako