BARCELONA, Bayern, Chelsea, Beşiktaş, Manchester City, PSG, Real Madrid na Tottenham tayari zilishafuzu hatua ya 16 bora lakini kuna timu nyingine 14 zinazowania nafasi nane zilizobaki katika michezo ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya itakayochezwa kesho na keshokutwa Jumatano.
Mambo ni magumu sana kwa baadhi ya vigogo, tazama jinsi hali ilivyo:
Zinazoweza kufuzu: Atlético Madrid, Basel, CSKA Moskva, Juventus, Leipzig, Liverpool, Manchester United, Napoli, Porto, Roma, Sevilla, Shakhtar Donetsk, Spartak Moskva, Sporting CP.
Ambazo haziwezi kufuzu: Anderlecht, APOEL, Borussia Dortmund, Celtic. Zitakazomaliza mkiani: Benfica, Feyenoord, Maribor, Monaco, Olympiacos, Qarabağ.
MECHI ZA KESHO JUMANNE
Kundi A: Manchester United (pointi 12) v CSKA Moskva (9), Benfica (0) v Basel (9)
Manchester United itafuzu ikiwa kileleni kama itapata pointi (na inaweza kufungwa 6-0 na bado ikafuzu). Kama Manchester itapoteza dhidi ya CSKA, na Basel ikashindwa kushinda dhidi ya Benfica, basi United na CSKA zitafuzu huku nafasi ya kwanza ikitegemea nani alivuna pointi nyingi zaidi walipokutana ‘head to head’ (United ilishinda 4-1 Urusi na itakuwa na uwiano mzuri zaidi wa mabao hata ikifungwa 4-1 kesho).
Kama CSKA na Basel zitashinda, basi nafasi mbili za juu itategemea ulinganifu wa nani alivuna pointi nyingi zaidi timu hizo tatu zilipokutana, ‘head to head’. Ikitokea hali hii, United watafuzu labda wafungwe 7-0, na watakuwa vinara labda wafungwe 5-0.
Basel watafuzu kama wakiwa na matokeo mazuri zaidi ya CSKA au kama timu zote zikifungwa ama kutoka sare, kwa sababu Basel wana pointi nyingi zaidi timu hizo zilipokutana ‘head to head’.
Kundi B: Bayern (12) v PSG (15), Celti c (3) v Anderlecht (0)
Paris na Bayern zote zilishafuzu, huku nafasi ya kwanza ikitegemea mchezo baina ya timu hizo. Paris ilishinda mchezo wa kwanza 3-0 na pia inaongoza kwa uwiano mzuri wa mabao, hivyo Bayern inatakiwa ishinde kwa tofauti y a m a b a o m a n n e ili imalize kinara.
Celtic na Anderlecht, m m o j a w ap o anaweza kumaliza katika nafasi ya tatu. Anderlecht walifungwa na Celtic 3-0 nyumbani, kwa hiyo Wabelgiji hao watalazimika kushinda kwa tofauti ya mabao matatu jijini Glasgow ili kufuzu Europa (kama wakishinda 3-0, Anderlecht watamaliza nafasi ya tatu kutokana na uwiano mzuri wa mabao walionao).
Kundi C: Roma (8) v Qarabağ (2), Chelsea (10) v Atlético (6)
Chelsea walishafuzu. Watathibitisha nafasi ya kwanza kwa ushindi au kwa matokeo yoyote yale kama Roma ikishindwa kushinda.
Roma itafuzu kwa ushindi, au kwa matokeo yoyote kama Atletico Madrid itashindwa kushinda. Kama Roma ikishinda, na Chelsea ikashindwa kushinda, basi Roma watakuwa vinara.
Atlético wenyewe, ili wamalize katika nafasi ya pili, wanatakiwa kushinda na kutegemea Roma haishindi (kama Atletico na Roma wakimali z a na pointi tisa, Atletico itafuzu kutokana na kuwa na pointi nyingi timu hizo zilipokutana ‘head to head’). Qarabağ haina mjadala, itamaliza ya mwisho.
Kundi D: Olympiacos (1) v Juventus (8), Barcelona (11) v Sporting (7)
Barcelona walishafuzu kama vinara. Juventus watafuzu kwa ushindi au kwa matokeo yoyote kama Sporting watashindwa kushinda (kama wakimaliza pointi sawa, Juve itafuzu kwa uwiano mzuri wa head-to-head).
Sporting lazima ishinde, na itatinga 16 bora kama ikishinda halafu Juventus ikashindwa kushinda. Olympiacos watamaliza mkiani.
MECHI ZA JUMATANO
Kundi E: Maribor (2) v Sevilla (8), Liverpool (9) v Spartak Moskva (6)
Liverpool inahitaji sare tu ili ifuzu, na itajithibitishia nafasi ya kwanza kwa ushindi, au kwa sare kama Sevilla isiposhinda. Kama Liverpool ikifungwa, itatupwa nje labda Sevilla nayo ifungwe (maana Liverpool itakuwa ya tatu kama timu zote zikilingana pointi, kutokana na uwiano wa mabao ya head to head).
Sevilla itafuzu kwa sare, au kwa matokeo yoyote kama Spartak isiposhinda. Sevilla itashika nafasi ya kwanza kama ikishinda halafu Liverpool isiposhinda.
Spartak itafuzu kwa ushindi lakini itashika nafasi ya tatu kwa matokeo yoyote. Kama Spartak ikishinda itamaliza kileleni labda Sevilla nayo ishinde. Maribor haiwezi kujikwamua mkiani.
Kundi F: Feyenoord (0) v Napoli (6), Shakhtar Donetsk (9) v Manchester City (15)
Man City walishafuzu kama vinara. Shakhtar watafuzu kama wataepuka kipigo au kama Napoli isiposhinda.
Napoli yenyewe lazima ishinde halafu itegemee Shakhtar ipoteze; katika mazingira hayo, Napoli itamaliza ya pili kwa faida ya head to head. Feyenoord haitaweza kutoka mkiani.
Kundi G: Porto (7) v Monaco (2), RB Leipzig (7) v Beşiktaş (11)
Beşiktaş wameshafuzu kama vin a r a . P o r t o watafuzu k a m a wakishinda
au ikiwa tu watalingana pointi na Leipzig kutokana na faida yao ya head to head.
Leipzig lazima ipate pointi nyingi zaidi ya Porto ili kumaliza ya pili. Monaco iliyofika nusu fainali msimu uliopita, haitatoka mkiani.
Kundi H: Real Madrid (10) v Dortmund (2), Tottenham (13) v APOEL (2)
Tottenham walishafuzu kama vinara kwa faida ya head to head dhidi ya Madrid. Madrid ilishafuzu kama mshindi wa pili. Dortmund na APOEL zitawania nafasi ya tatu. Ikiwa mwisho wa siku timu hizo zitalingana pointi, Dortmund itafuzu kutokana na uwiano mzuri wa mabao katika mechi zote.
Tupe Maoni Yako