Tuesday, December 19, 2017

Mawingu Tz

Taarifa Njema Kutoka Yanga Jioni Ya Leo Kuhusu Kamusoko

Baada ya matibabu ya umakini mkubwa, Kiungo Thabani Kamusoko wa Yanga, anaweza kuanza mazoezi kesho.

Habari kutoka ndani ya Yanga zinaeleza, Kamusoko yuko katika hali nzuri ya kuanza mazoezi ya taratibu.

“Hali yake imaimarika na anaweza kuanza mazoezi ya kukimbia lakini taratibu,” kilieleza chanzo.

“Matibabu yalikuwa ya umakini mkubwa na uongozi ulilisimamia hilo kwa kushirikiana na baadhi ya wanachama wa klabu walioonyesha moyo wa kizalendo kwa klabu,” kilieleza chanzo.


Yanga imekosa huduma ya Mzimbabwe huyo kwa zaidi ya miezi miwili sasa lakini Kocha George Lwandamina ameendelea kupambana na kikosi chake kiko katika nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu Bara.

Tupe Maoni Yako