Tuesday, December 12, 2017

Mawingu Tz

Taarifa Mpya Kutoka Yanga Jioni Ya Leo

Klabu ya YANGA leo imethibitisha kuwa siku ya jumamosi itakuwa na mchezo wa kirafiki kati yake na Polisi Tanzania Inayoshiriki ligi daraja la Kwanza Tanzania Bara.
Afisa habari wa timu ya Yanga Dismas Ten amesema kuwa mchezo huo utachezwa katika dimba la uwanja wa Taifa Dar Es Salaam ikiwa ni mchezo wa Kwanza kwa timu zinazoshiriki ligi kuu na daraja la kwanza toka uwanja huo ulipofungwa kwaajili ya Marekebisho kadhaa.
WACHEZAJI WALIOTOKA KILI STARS
Dismas Ten msomaji wa Kwataunit.com amesema pia kuanzia kesho wanategemea kuanza kuripoti kwa wachezaji waliokuwa katika timu ya Taifa ya Tanzania Bara ” Kilimanjaro Stars ”
Yanga leo walikuwa na mazoezi ya Gym na kesho wataendelea na Program nyingine za Mazoezi wakijiandaa na Ligi na Mashindano mengine yaliyombele yao.

Tupe Maoni Yako