Tuesday, December 12, 2017

Mawingu Tz

Jembe La Mtibwa Sugar Mbioni Kutua Simba

Kiungo mshambuliaji wa Mtibwa Sugar, Mohamed Issa 'Banka' yupo mbioni kukamilisha mpango wa kujiunga na klabu ya Simba, ambayo imeonyesha kwenda resi kwa ajili ya kumsajili katika kipindi hiki dirisha dogo.
Meneja wa mchezaji huyo Jamali Kisongo, amesema  amekuwa akikutana mara kwa mara na viongozi wa klabu ya Simba, kwa ajili ya kufanya mazungumzo na timu hiyo kwa ajili ya kumsajili mchezaji huyo ambaye kwa sasa amekuwa gumzo nchini.
"Simba wapo kwenye wakati mzuri kumchukua kwasababu wamekuja na tumezungumza nao zaidi ya mara mbili na ukweli mambo yanakwenda vizuri kama wakiendelea hivi wanaweza kumchukua Banka," amesema Kisongo.
Kiongozi huyo amesema awali Yanga walikuwa wakimtaka mchezaji huyo lakini wamekuwa kimya tofauti na wenzao Simba ambao licha ya kuongea kupitia vyombo vya habari lakini wameonyesha kwa vitendo kama kweli wanamuhitaji mchezaji huyo kwa kukutana naye yeye kama Meneja wa mchezaji.
Mohamed Issa 'Bank' amekuwa kwenye kiwango bora hivisasa kutokana na kazi nzuri anayoifanya kwenye klabu yake ya Mtibwa na timu ya taifa ya Zanzibar ambayo inashiriki michuano ya kombe la Chalenji huko nchini Kenya.

Tupe Maoni Yako