Friday, December 8, 2017

Mawingu Tz

MUHIMU:Taarifa Mpya Kutoka Simba Asubuhi Hii Leo Dec 8 2017


Uongozi wa Klabu ya Simba, umewapa ofa wachezaji wake wa kimataifa ya kuendelea kupumzika mpaka michuano ya Chalenji itakapomalizika kutokana na kusimama kwa Ligi Kuu Bara.

Simba baada ya kucheza mechi yake ya mwisho ya ligi dhidi ya Lipuli FC, Novemba 26, mwaka huu na kutoka sare ya 1-1, ikawapa likizo ya wiki moja wachezaji wake wote.

Likizo hiyo ilipomalizika, wachezaji wazawa ambao hawapo na timu zao kwenye Chalenji, walianza mazoezi Jumatatu ya wiki hii, lakini wale wa kimataifa wote wakiendelea kuwepo kwenye mapumziko hadi hapo baadaye.

Mratibu wa Simba, Abass Ally amesema wachezaji hao wanatarajia kurejea kwenye kikosi hicho kwa nyakati tofauti wakitoka kwenye mapumziko.


“Wachezaji wetu wa kigeni wapo mapumzikoni kwa sasa na watarejea muda wowote kwa nyakati tofauti kwa sababu hiki ndiyo kipindi pekee cha wao kupumzika maana baada ya hapo hakuna mapumziko tena hata kuondoka kwao waliondoka kwa siku tofauti.

“Ndiyo maana hata kocha mwenyewe hayupo yuko kwenye mapumziko kwao ndiyo maana tunaendelea na wachezaji wa hapa nyumbani ambao hawako kwenye timu ya taifa, ndiyo wanafanya mazoezi,” alisema Abbas.


Ikumbukwe Simba ina wachezaji wa kigeni kama Nicholus Gyan na James Kotei (Ghana), Emmanuel Okwi na Juuko Murshid (Uganda), Haruna Niyonzima (Rwanda), Method Mwanjale (Zimbabwe) na Laudit Mavugo (Burundi).

SOURCE: CHAMPIONI

Tupe Maoni Yako