Monday, December 11, 2017

Mawingu Tz

Mourinho Awaponda City...Asema Refa Kawabeba Tu

Kila mwanahabari duniani wakati wa mchezo mkubwa ambao unamhusu Jose Mourinho huwa wanamtafuta ili kufahamu nini maoni yake, ndio na Mourinho amekuwa bora kuwapa wanahabari kile wanachokitaka.
Jose Mourinho amesema City hawakupaswa kushangilia kutokana na aina ya mabao ambayo wamefunga, huku akidai kwamba mabao yote mawili ya Manchester City yalionekana yalikuwa ya bahati tu.
Mourinho amehoji kwamba kama Manchester City waliwashika sana kama watu wanavyodai mbona golikipa wao Ederson ndio golikipa aliyeokoa hatari zaidi (Shambulizi la Lukaku na Mata) kuliko golikipa wao.
Mourinho amempongeza refa wa mchezo huo Michael Oliver kwa alivyokuwa mtulivu katika mchezo huo lakini akamponda kwa kuwanyima penati dakika za mwisho ambapo Ander Herrera alionekana akiangushwa katika eneo la 18.
Manchester City sasa wanakuwa wamefikisha alama 46 baada ya mchezo wa jana zikiwa ni alama 11 mbele ya Manchester United jambo ambalo tayari linawapa nafasi kubwa kuwa mabingwa wa EPL msimu huu.

Tupe Maoni Yako