Kocha wa Lipuli FC na nahodha wa zamani wa Simba na timu ya taifa, Taifa Stars, Selemani Matola amesema kitendo cha Yanga kumsajili straika Yohana Nkomola, basi imelamba dume.
Matola ametoa kauli hiyo baada ya kusikia Yanga imemsajili Nkomola ambaye alifanya vizuri katika michuano ya vijana ya Kombe la Mataifa ya Afrika chini ya miaka 17 nchini Gabon, mwaka huu.
Kwa sasa, Nkomola yupo Kenya na kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars kinachoshiriki Kombe la Chalenji. Mshambuliaji huyo, amesaini mkataba wa miaka miwili hivi karibuni kuichezea Yanga
akitokea kikosi cha U20 cha Azam FC.
Matola alisema anafurahishwa na usajili unaondelea kufanywa na Yanga kwa kusajili wachezaji wengi
vijana wenye pumzi na kasi.
“Nimeshtushwa na usajili wa Nkomola kwenda Yanga, hapa Yanga imefanya bonge la usajili, kiukweli huyu ni mchezaji mzuri na chipukizi anayekuja kwa kasi hivi sasa katika soka la Tanzania.
“Niwe muwazi Yanga wanafanya vizuri kwenye usajili wao na wanatengeneza vizuri timu yao ambayo ninakuhakikishia baada ya mwaka mmoja watakuwa tishio,” alisema Matola. Matola alisema, usajili wa vijana ndiyo wa kisasa akiamini baada ya mwaka mmoja Yanga itakuwa tishio kutokana na kuwepo vijana wengi wanaoutaka mpira muda wote
wakiwa uwanjani.
Aliongeza kuwa, Nkomola ni kati ya washambuliaji aliokuwa
akiwafuatilia kwa ukaribu kutokana na uwezo wa kufunga na kutengeneza nafasi ya kufunga mabao.
-Salehe jembe
Tupe Maoni Yako