Tuesday, December 12, 2017

Mawingu Tz

Kabunda Awachomoa Simba Sh. 60 Mil


KLABU ya Mwadui FC, imemwachia winga wao, Hassan Kabunda kwenda Simba lakini kwa sharti moja tu, walipwe Sh. 30 mil na wakishindwa waachane na mchezaji wao.
Simba inatakiwa kutoa jumla ya Sh 60 mil ambapo Sh. 30 mil zitakwenda Mwadui kwa ajili ya kuvunja mkataba na Sh. 30 mil nyingine ni za usajili wa Kabunda.
Hata hivyo, habari za ndani ni kwamba, Simba imekubali kutoa kiasi hicho cha pesa kuhakikisha wanamsajili Kabunda ambaye leo hii, amesafiri kutoka Shinyanga kwenda Dar es Salaam kwa ajili ya kuweka sawa mpango huo.
Mtu wa karibu wa mchezaji huyo alisema: "Mwadui wako tayari kumwachi Kabunda aende Simba, lakini
wanachotaka ni Sh. 30 mil tu wamalizane, hivi ninavyokwambia Kabunda amesafiri leo kutoka Shinyanga
kwenda Dar es Salaam kwa ajili ya kumaliza suala hilo."
Simba inamuhitaji Kabunda kwa ajili kukiboresha kikosi chao kwenye safu ya winga ambayo inachezwa zaidi na Shiza Kichuya.

Tupe Maoni Yako