Tuesday, December 12, 2017

Mawingu Tz

Huyu CONTE Vipi? Awakatisha Tamaa Kabisa Mashabiki Wa Chelsea

Meneja huyo wa Kiitaliano ameanza kupata hofu kuwa mabingwa hao watetezi watashindwa kufuzu nne bora msimu huu kutokana na ushindani.
Meneja wa Chelsea, Antonio Conte ameionya timu yake kuwa watakabiliwa na ushindani mkubwa kutinga nne bora Ligi Kuu Uingereza msimu huu kufuatia kichapo cha kushtukiza kutoka kwa West Ham United Jumamosi.
Mabingwa hao watetezi wamefungwa na Wagonga nyundo wanaohaha mkiani kwenye uwanja wa London na kujikuta wakiachwa kwa pengo la alama 14 na Manchester City, ingawa Manchester United, Liverpool na Arsenal pia zimepoteza pointi katika mechi za wikiendi.
Chelsea inabaki nafasi ya tatu kwani timu nyingi zimeshindwa kupata matokeo mazuri wikiendi, lakini Conte amesisitiza kuwa kipaumbele chao ni kuhakikisha wanafuzu kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa msimu ujao baada ya kukata tamaa kutetea ubingwa.
"Kuna tatizo kwenye hii ligi. Kuna timu sita za juu na kuna nafasi nne tu kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa na nafasi mbili kwa ajili ya Ligi ya Europa," aliwaambia waandishi.
"Tuna malengo, pia kama Manchester City wana pointi nyingi juu yetu, tuna lengo moja ambalo ni kujitahidi kutinga nne bora na kucheza Ligi ya Mabingwa. Bila kusahau, miaka miwili iliyopita Chelsea walikosa kushiriki, msimu uliopita hatukucheza michuano ya Ulaya.
"Shabaha yetu ni kucheza ligi. Narudia, tuna malengo yetu na ni lazima tupate nafasi katika nne bora kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa.
"Usisahau kwamba msimu uliopita Arsenal na Manchester United walikuwa nje ya michuano ya Ligi ya Mabingwa, kisha United wakatwaa taji la Ligi ya Europa, lakini vinginevyo Manchester United na Arsenal zingekosa. Shabaha hii ni muhimu sana kwangu, kwa wachezaji na kwa kila mmoja. Narudia, si kazi rahisi kutinga nne bora."
Chelsea wataikabili Huddersfield Town kwenye uwanja wa John Smiths Jumanne usiku wakilenga kurudi kwenye njia za ushindi.


Tupe Maoni Yako