Thursday, November 30, 2017

Mawingu Tz

Omog Huyooo, Masoud Djuma Kwa Raha Zake Simba


KOCHA Mkuu wa Simba, Joseph Omog, ameondoka nchini jana usiku kwenda kwao kwa ajili ya mapumziko baada ya kusimama kwa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa wiki tatu, huku majukumu yake yote akiyaacha kwa msaidizi wake, Massoud Djuma.
Omog ameondoka huku akiwa tayari amewapa viongozi wake mapendekezo ya usajili wa dirisha dogo.Katika ripoti yake, Omog amependekeza marekebisho yafanywe kwenye safu ya ulinzi, kipa mmoja, beki wa kati na straika mmoja.

Wakati Omog akiondoka na kuacha ripoti hiyo, wachezaji wa timu hiyo wamepewa mapumziko ya wiki moja, kuanzia Jumatatu hadi Jumapili ya wiki hii ambapo watarejea uwanjani kuanza mazoezi rasmi kuanzia Jumatatu ijayo.
Kikosi cha Wekundu wa Msimbazi hao kitaanza mazoezi yake rasmi kikiwa chini ya Mrundi, Djuma, kujiandaa na mwendelezo wa Ligi Kuu Bara raundi ya 12.
Ligi Kuu Bara imesimama kupisha michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Cecafa Challenge Cup) kwani baadhi ya wachezaji wa klabu kadhaa wamejiunga na timu zao za taifa kuzitumikia katika kipute hicho kitakachoanza Desemba 3, mwaka huu nchini Kenya.

Simba imekwenda kupumzika ikiwa bado inaongoza Ligi Kuu ikiwa kileleni na pointi 23, ikifuatiwa na Azam waliolingana nao pointi, wakitofautiana kwa idadi ya mabao ya kufunga.
-Dimba

Tupe Maoni Yako