Thursday, November 30, 2017

Mawingu Tz

Maskini Emmanuel Okwi!!

Mshambuliaji wa Simba na kinara wa ufungaji katika Ligi Kuu Bara, Emmanuel Okwi ameachwa katika kikosi cha Uganda kitakachoshiriki mashindano ya Chalenji.
Wakati Okwi mwenye mabao nane katika kikosi cha Simba akiachwa Mganda mwenzake beki Juuko Murushid ndiye mchezaji pekee anayecheza nje ya Uganda aliyeitwa Cranes.
Kocha wa zamani wa Simba, anayefundisha Cranes, Moses Basena ameita wachezaji 26 kambini watakaopungua na kubaki 23 kabla ya safari ya Nairobi Jumamosi hii wakati mashindano yatafunguliwa Jumapili Desemba 3.
Okwi bado hajarejea dimba tangu apete majeraha akiwa na timu ya Taifa wakati wa maandalizi ya mchezo wa kusaka tikeki ya fainali ya kombe la dunia dhidi ya Congo.

Tupe Maoni Yako