Thursday, November 30, 2017

Mawingu Tz

MO Dewji Kubanwa Na Serikali Kwenye Kuinunua Simba,Waziri Mwakyembe Afunguka Haya

Waziri wa Habari,Utamaduni, sanaa na Michezo Harrison Mwakyembe ameweka wazi kuwa kuna sheria ambayo imepitishwa October 27 Mwaka huu (2017) ambayo inazuia mtu mmoja kumiliki hisa zaidi ya asilimia 49.
Katika sheria hiyo  inamzuia mwekezaji kuwa na sauti ya mwisho kwenye klabu ambayo imeanzishwa na wanachama, Akiongea kupitia EFM Waziri wa Habari,Utamaduni, sanaa na michezo Harrison Mwakyembe amesema
VILABU AMBAVYO VIMEANZISHWA  NA WANACHAMA VINATAKIWA KUWAACHIA NA WAWEKEZAJI WA SEKTA BINAFSI LAKINI WAWEKEZAJI WA SEKTA BINAFSI HAWATAKIWI KUMWACHIA MWEKEZAJI MMOJA AKAMILIKI KLABU ILIYOANZISHWA NA WANACHAMA.
Na hata ikitokea akamiliki asilimia zisizozidi asilimia 49 basi Mtu huyo hatatakiwa kuwa ndiye mwenye Sauti ya mwisho kwenye Klabu iliyoanzishwa na wanachama.
KLABU ILIYOANZISHWA NA WANACHAMA ISIPOTEZE SIFA YA WANACHAMA KUWA NA SAUTI KATIKA KLABU YAO LAKINI UWEKEZAJI NI MUHIMU NDIYO MAANA TUNARUHUSU ASILIMIA 49 LAKINI MWEKEZAJI HATAKIWI KUWA NA SAUTI YA PEKE YAKE.
Alimaliza Mwakyembe, ambaye alisisitiza vilabu pekee ambavyo vinaweza kufanya jambo kama hilo bila pingamizi ni vilabu vya watu binafsi,  Ili kupata mwisho wa sakata hili endelea kuwa karibu nasi kila mara kila wakati.

Tupe Maoni Yako